Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
WAZIRI MKUU KUANZA ZIARA YA KIKAZI TANGA KESHO, KUZINDUA MIRADI YA BIL.700.5

WAZIRI MKUU KUANZA ZIARA YA KIKAZI TANGA KESHO, KUZINDUA MIRADI YA BIL.700.5

 


NA AMINA SAIDI, MATUKIO DAIMA MEDIA, TANGA.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Mwigulu Nchemba anatarajiwa kuanza ziara ya kikazi mkoani Tanga kesho, Ijumaa, Februari 13, 2026, kwa ajili ya kukagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilaya zote za mkoa huo.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa, Waziri Mkuu atapokelewa rasmi majira ya asubuhi katika eneo la Mkata, Wilaya ya Handeni, ambapo ndipo itakuwa lango kuu la kuanzia ziara hiyo muhimu mkoani hapa.

Ziara hii inalenga kukagua maendeleo ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa na serikali, ikiwemo

   Ukaguzi wa barabara na madaraja yanayounganisha wilaya za mkoa huo,

  Uzinduzi wa vituo vya afya na majengo mapya ya shule yaliyokamilika

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Batlda Buriani amewataka wananchi wa Mkata na maeneo ya jirani kujitokeza kwa wingi kumpokea kiongozi huyo.

 Alibainisha kuwa ujio wa Waziri Mkuu ni fursa kwa mkoa kuonyesha hatua kubwa zilizopigwa katika kutekeleza ilani ya chama tawala na kutatua changamoto za wananchi.

"Tumejipanga vyema kuhakikisha ziara hii inafanikiwa kuanzia Mkata mpaka wilaya ya mwisho,Miradi yote iko tayari Kwa ukaguzi na mingine Kwa ajili ya kuzinduliwa ili ianze kutoa huduma rasmi"Alisema Buriani.

  Waziri Mkuu anatarajiwa  kuanza ziara yake katika Wilaya ya Handeni kabla ya kuelekea wilaya nyingine za mkoa huo.

Ziara hii inakuja wakati mkoa wa Tanga ukiwa katika kasi kubwa ya mabadiliko ya kiuchumi, hususan kupitia uboreshaji wa bandari na viwanda.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3