WAANDISHI IRINGA WAPATA AJALI
Waandishi hao walipata ajali hiyo Alhamisi February 5 majira ya saa 9 Alasiri katika kijiji cha Idodi kwenye barabara kuu ya Iringa -Msembe baada ya gari walilokuwa wakisafiria kuparamia kifusi kilichokuwa kimemwagwa barabarani kwa ajili ya matengenezo ya barabara ya lami eneo hilo.
Mashuhuda wa tukio hilo wamezungumza na Matukio Daima kuwa chanzo cha ajali ni kifusi na dereva kushindwa kulimudu gari lake.
Hata hivyo waandishi waliopata ajali hiyo walikimbizwa kituo cha afya Idodi kupatiwa matibabu na baadae kuhamishiwa Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa ambako baadhi yao waliruhusiwa baada ya kutazamwa afya zao na waandishi wanne wamelazwa kwa matibabu zaidi Katika ajali hiyo hakuna kifo. Baadhi ya waandishi wa habari mkoani Iringa wamepata ajali ya gari leo Februari 5, 2026, wakirejea kutoka sherehe za Maadhimisho ya Miaka 49 ya Kuzaliwa kwa CCM zilizofanyika Kata ya Idodi, Wilaya ya Iringa.
Katika gari hilo la waliokuwepo ni pamoja na Zuhura Zukheri (Abood Media),Frank Leonard(Habari Leo) Denis Mlowe (Fullshangwe Media); Clement Sanga (Channel Ten),Herieth Molla (Mkombozi Tv) Juma Mpiga picha wa kujitegemea,mwenezi wa CCM mkoa wa Iringa Joseph Lyata na Dereva wa gari hiyo ,Huku mkurugenzi wa Matukio Daima Media Francis Godwin akinusurika ajali hiyo kwa kushindwa kupata gari hilo wakati wa kurudi na kubadili usafiri.
Matukio Daima Media ilishuhudia jitihada kubwa za viongozi wa chama na serikali ambao wakati wote walikuwa jirani na majeruhi hao kufuatilia maendeleo yao pamoja na kutoa pole.

