SMAUJATA WAFUNDWA KUHUSU USTAARABU NA ITIFAKI
Taasisi ya Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania SMAUJATA Wamepatiwa mafunzo ya Protocol and Etiquette ( Ustarabu na Itifaki za Viongozi) Maadili na Uzalendo kwa watumishi ili waboreshe utendaji kazi wao.
Katika kuhakikisha taasisi zinajengewa uwezo wa kiimadili katika kazi Mtaalamu wa Kidiplomasia, Uongozi na maadili ndugu Omary Abdull Punzi amewelekeza na kuwakumbusha taasisi ya SMAUJATA katika mafunzo yaliyoandaliwa na taasisi hiyo kuanzia tarehe Februari 7 hadi 8 mwaka huu katika Ukumbi wa Chuo Cha VETA Keko Dar es Salaam.
Mafunzo hayo yaliyofunguliwa na ndugu Salehe Omary Kaimu Mkuu wa Chuo cha VETA akimwakilisha mkuu wa chuo hiko na kufungwa na Fredrick Nelson Rwegasira - Makamu Mwenyekiti SMAUJATA
Aidh mafunzo hayo yalijikita katika
Itifaki na Ustarabu wa Viongozi sambamba na maadili.




