Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
SERIKALI YAIMARISHA MFUMO WA UTAFUTAJI NA UOKOAJI MAJINI

SERIKALI YAIMARISHA MFUMO WA UTAFUTAJI NA UOKOAJI MAJINI

 

Na Hamida Ramadhan, Matukio Daima Media Dodoma

SERIKALI kupitia Wizara ya Uchukuzi imeweka kipaumbele kikubwa katika kulinda maisha ya wananchi na mali zao kwa kuimarisha mifumo ya utafutaji na uokoaji majini ili kuhakikisha hakuna mwananchi anayepoteza maisha wakati akijitafutia riziki ndani ya maji na hata pale ajali zinapotokea kunakuwepo na uwezo wa haraka wa kumuokoa mhusika. 

Waziri wa Uchukuzi Makame Mbarawa ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari Februari Mosi jijini Dodoma wakati akieleza Ahadi za Rais Samia kwa siku 100 tangu kuapishwa kwake . 

 Waziri huyo amesema hatua zinazochukuliwa ni sehemu ya ahadi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan za kuboresha usalama wa usafiri, huduma za afya na ustawi wa wananchi hususan wanaoishi visiwani na maeneo ya mwambao. 

Ameeleza kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha ahadi hizo zinatekelezwa kwa vitendo kwa kuwekeza katika miundombinu, vifaa vya kisasa na rasilimali watu.

"Katika kipindi cha siku 100 zilizopita, Serikali imekamilisha ujenzi wa Kituo cha Kuratibu Utafutaji na Uokoaji cha Kikanda katika Ziwa Victoria mkoani Mwanza ambacho kitaimarisha usalama wa usafiri wa majini kwa kutumia mifumo ya kisasa ya mawasiliano, TEHAMA na vifaa vya uokoaji hali itakayoongeza ufanisi wa uokoaji pale majanga yanapotokea, " Amesem


Aidha Wizara ya Uchukuzi imenunua boti maalum ya wagonjwa kwa ajili ya Ziwa Victoria ambayo tayari imewasili na iko tayari kutoa huduma kwa wananchi, boti hiyo ikielezwa kuwa ni kama hospitali inayotembea majini na itarahisisha upatikanaji wa huduma za dharura kwa wakazi wa visiwa na maeneo ya mwambao wa ziwa.


Sambamba na hatua hiyo, Serikali imenunua boti nne za utafutaji na uokoaji ambazo zimeanza kutumika katika Ziwa Tanganyika, Ziwa Victoria na Ukanda wa Bahari ya Hindi katika eneo la Tanga, hatua ambayo imeongeza uwezo wa Taifa katika kukabiliana na majanga ya majini na kuimarisha zaidi usalama wa usafiri wa maji nchini.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3