RAIS WA CONGO BRAZAVILLE (82) KUTANGAZA KUWANIA TENA URAIS
Akiwa na umri wa miaka 82, Madarakani kuanzia 1979 hadi 1992, kisha 1997 hadi leo, Rais Denis Sassou Nguesso anajiandaa kutangaza rasmi, Alhamisi hii, Februari 5, kuwania Urais katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Machi 15, 2026.
Sassou Nguesso aliyezaliwa 1943 na alikuwa afisa wa Jeshi ambapo alijiunga na Jeshi 1960 muda mfupi kabla Jamhuri ya Congo kupata Uhuru wake.
Baadaye alikuwa Mkuu wa idara ya Ujasusi Jeshini. Katika miaka ya sitini alishiriki kwenye Mapinduzi ya Kijeshi nchini humo. Aliwahi kuwa Waziri wa Ulinzi akiwa na umri wa miaka 32.
Akiwa na Chama chake cha PCT alishinda Uchaguzi Mkuu wa 1979. Akashinda tena Uchaguzi wa 1984 na baada ya miaka mitano akarejea tena Ikulu kupitia Uchaguzi wa 1989.
Alianzisha mfumo wa siasa za vyama vingi mwaka 1990. Akashindwa kwenye Uchaguzi wa 1992

