Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
NCAA YAZINDUA CHAPA MPYA YA DESTINATION NGORONGORO.

NCAA YAZINDUA CHAPA MPYA YA DESTINATION NGORONGORO.

 


Na,Jusline Marco;Arusha

Mamlaka ya hifadhi ya eneo la Ngorongoro imezindua Utambulisho Mpya wa Chapa ya “Destination Ngorongoro” inayoashiria mwanzo mpya wa maajabu ya Ngorongoro ambayo kwa miongo mingi imekuwa ikivutia dunia kwa uzuri wake wa kipekee.




Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika kwenye eneo la Ndugu lililopo ndani ya hifadhi ya Ngorongoro, Kamishna wa Uhifadhi mamlaka hiyo Abdul-Razaq Badru ameeleza kuwa kabla Ngorongoro haijawa kivutio cha utalii kinachotambuliwa duniani, ilikuwa ni sauti yenye mwito wa uhai unaounganisha Wanyamapori, utamaduni, ardhi, historia ya mwanadamu, malikale, mazingira na maumbo mbalimbali yanayoiakisi dunia ilipojikunja na kuunda Kasoko ya Ngorongoro.

“Katika dunia ambayo ushindani wa vivutio vya utalii ni mkubwa unaozidi kuwa na Faru, tembo na visukuku pekee, Ngorongoro imeamua kujipambanua zaidi kwa mwito wenye dhamana na wajibu ndio maana tunawatambulisha rasmi muonekano mpya wa chapa ya 'Destination Ngorongoro' kwa kufanya maboresho ya namna Ngorongoro inavyojitambulisha kwa dunia na kwa wageni kwa umahiri na muonekano ulioboreshwa” amefafamua kamishna Badru.


Kamishna Badru akiwa ameongoza na Menejimenti ya mamlaka hiyo na wadau mbalimbali wa sekta ya utalii amesema moja ya maajabu ya kipekee ya asili duniani ni tukio la kuzaliana kwa nyumbu eneo la Ndutu ambapo kila baada ya saa moja takribani ndama 80,000 huzaliwa. 

Ameongeza kuwa katika Bonde la Olduvai na Laetoli, historia na nyayo za kwanza za binadamu zilipatikana zikitukumbusha kuwa Ngorongoro si hadithi ya wanyamapori pekee, bali ni Chimbuko la binadamu, hii ni ishara kuwa Ngorongoro ni maajabu yanayopaswa kusimuliwa hatua kwa hatua na Ngorongoro sio tu unatazamwa bali inabaki na kuishi mioyoni mwa watu.


Amebainisha kuwa maboresho ya chapa ya Ngorongoro hayapo kwenye muonekano pekee bali pia yanasimuliwa kwa hadithi za Ngorongoro ili wageni wa mataifa mbalimbali wanapofika Ngorongoro waelewe zaidi kuhusu chimbuko na asili yake.

Amebainisha kuwa mwaka 2026 utakuwa Mwaka wa Maajabu,chini ya kauli mbiu isemayo “Wonders Are Calling” ambayo itatekelezwa kwa awamu ikifichua maajabu ya Ngorongoro kwa kila msimu.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3