Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
NAIBU WAZIRI UMMY AZIBANA HALMASHAURI KUHUSU MKOPO WA WATU WENYE ULEMAVU

NAIBU WAZIRI UMMY AZIBANA HALMASHAURI KUHUSU MKOPO WA WATU WENYE ULEMAVU

 

MATUKIO DAIMA MEDIA.

MOSHI. 

HALMASHAURI nchini zimetakiwa kuzingatia mikopo inayoombwa na Watu wenye ulemavu na kuwapa fedha kulingana na kiwango wanachoomba ili kuweza kuleta tija na kutimiza lengo lililokusudiwa na Serikali. 

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge, Uratibu na Watu wenye ulemavu, Ummy Nderiananga alipozunguma na Watu wenye ulemavu katika halmashauri ya Moshi na manispaa ya Moshi. 

Naibu Waziri huyo alishangazwa na kitendo cha Watu wenye ulemavu kupewa fedha tofauti na kiwango alichoomba kwenye mkopo wa asilimia mbili ya mapato ya ndani ya halmashauri hali ambayo inapelekea kushindwa kutekeleza adhima aliyoombea mkopo huo. 

"Mtu ameshaleta wazo lake na mchanganua wa fedha anazohitaji sasa unapompa nusu ya hiyo hela au robo unategemea kweli biashara aliyokuwa anategemea kwenda kuianza atafanya au mnataka achukue hizo fedha akale alafu akishindwa kurejesha mnaenda kumkamata hii sio sawa" Alisema Naibu Waziri Ummy. 

Awali akisoma taarifa kwa Naibu Waziri, Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii wilaya ya Moshi, Stella Magori alisema kuwa, halmashauri ya Moshi ina jumla ya watu wenye ulemavu 154 ambapo katika mwaka wa fedha 2024/2025 halmashauri ilitoa mkopo wa milioni 60.4 kwa vikundi 15 vya watu wenye ulemavu. 

Kwa upande wao baadhi ya Watu wenye ulemavu walielezea changamoto wanazokabiliana nazo katika uombaji wa mikopo hiyo.

MWISHO.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3