MSIWAFUMBIA MACHO WATUMISHI WANAMKWAMISHA RAIS DKT SAMIA KUTEKELEZA ILANI -ARIF ABRI
NA MATUKIO DAIMA MEDIA.
Mjumbe wa mkutano Mkuu wa chama cha mapinduzi (CCM )Taifa Arif Abri amewataka viongozi wa CCM kusimamia utekelezaji wa Ilani ya CCM na kuwakemea watendaji wasipwajibika kumsaidia Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kusimamia ilani .
Abri alitoa agizo hilo leo wakati akifungua kikao cha baraza la kumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Iringa vijijini na kusema kuwa endapo watakuta miradi inasuasua ni jumuku lao kuiambia serikali ili itekeleze kwa wakati na wasisite kukemea viongozi wa serikali wazembe.
"Watumishi wa umma wanatekeleza ilani ya CCM na wanalipwa kodi za wananchi hivyo lazima wawajibike kusimamia miradi hiyo maana wakati wa kampeni tunaoulizwa ni sisi Viongozi wa CCM waliotuchagua hivyo lazima tuwabane sasa kusimamia miradi ili kuondoa maswali kwa wananchi wakati wa kampeni"
Abri alisema kuwa Rais Samia aliahidi katika kipindi cha siku 100 kuhusu bima ya afya kwa wote na tayari ametekeleza ahadi yake yake hiyo na sasa bima ya afya kwa wote inatolewa kwa kujumuiya kaya ya watu sita.
“Bima ya afya kwa wote itawasaidia wananchi kupata huduma ya afya bora na katika bima hii mama mjamzito ataweza kuitumia bila malipo, serikali pia inagharamia makundi yenye wahitaji kama vile watoto, wazee na wamama wajawazito”alisema
Alisema kuwa lengo la jumuiya ya wazazi ni kuwajenga jamii bora ya vijana hivyo amewaomba wazazi kushuka chini kuwalea vijana wawe na maadili na uzalendo wanchi yao na kuacha kufanya matukio ya uvunjifu wa amani.
“Jumuiya ya wazazi ndio nguzo ya malezi ya chama cha mapinduzi ya jumuiya zote zinazohusu malezi kuanzia ngazi ya familia hadi ngazi ya uongozi hivyo ni vyema tukajikita katika kuwalea watoto katika misingi iliyo bora ili kuwa na vijana wanaolipenda taifa na kuendeleza uzalendo”alisema
Katika hatua nyingi Mjumbe huyo wa mkutano mkuu wa CCM Taifa Arif Abri katika kuunga mkono jitihada za jumuiya hiyo kuwa na miradi yake ya kiuchumi amechangia kiasi cha Tsh Milioni 2.5 ili kununua viwanja vya kujenga kitega uchumi eneo la stendi ya Halmashauri ya wilaya ya Iringa vijijini itakayojengwa Migori .TAZAMA HOTUBA NZIMA YA ARIF ABRI BOFYA LINK HIIAkizungumza mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Iringa vijijini Michael Mario Kihongo amewashukuru wananchama wa ccm kwa kuendelea kukiamini chama hicho kwa kusimamia miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali.
“Chama cha Mapinduzi kinasimamia na kutekeleza miradi mbalimbali kama vile barabara, afya, maji na kingine mingi ambayo ni ahadi ya Rais samia kwa wananchi wake”alisema
Akizungumza Kaimu katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Iringa vijijini Sophia Nyalusi alisema kuwa wanaishukuru jumuiya ya wazazi kwani mapaka sasa hawajapata changamoto yeyote ya watoto kuto kulipoti shuleni.
“Jumuiya ya wazazi kupitia kata za wilaya hiyo zimefanya kazi kubwa ya kuelemisha wazazi kuwapeleka watoto shule na kujua umuhimu wa shule”
Awali akisoma taarifa fupi ya jumuiya ya wazazi katibu wa wazazi wilaya hiyo Anitha Magelanga alisema kuwa katika upande wa maeneo ya uwekezaji walifanikiwa kupata viwanja vitatu ambavyo bado havijalipiwa.
Alisema jumuiya hiyo pia ina mradi wa ujenzi wa nyumba ya mtumishi ambapo tayari wana matofali na wanakabiliwa na changamoto ya vifaa vya ujenzi kutokamilika ili ujenzi huo uweze kukamilika.








































