Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
MNEC KIGOMA ATAKA USHIRIKISHWAJI JAMII KWENYE MIRADI

MNEC KIGOMA ATAKA USHIRIKISHWAJI JAMII KWENYE MIRADI


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

Mjumbe wa halmashauri kuu ya Taifa ya CCM Abdulkadri Mushi ametaka ushirikishwaji wa viongozi wa serikali za mitaa, mabalozi na viongozi wa matawi wa chama tawala na wananchi ili waweze kushiriki kwenye utekelezaji wa miradi na kuilinda miradi hiyo.

Mushi alisema hayo akiongoza kamati ya siasa ya Halmashauri kuu ya CCM mkoa Kigoma kutembelea na kukagua miradi mbalimbali inayoyekelezwa katika halmashauri ya wilaya Kigoma na kubainisha kuwa ushirikishwaji wa wananachi na viongozi wa serikaali za mitaa una maana kubwa katika kuwafanya watu hao kuuona mradi kama sehemu yao.

Akiwa katika mradi wa shule ya sekondari ya Amali ya Halmashauri ya wilaya Kigoma Mjumbe huyo wa halmashauri kuu ya Taifa ya CCM alisema kuwa wakati mwingine hujuma katika miradi inatokana na wananchi na viongozi wa kata na matawi kutoshirikishwa na hivyo kuona miradi hiyo siyo sehemu ya maisha yao na kusababisha baadhi ya watu kujinufaisha binafsi kwa kuhujumu miradi hiyo.

Akiuelezea mradi huo alisema kuwa unatekeleza kwa vitendo Imani ya uchaguzi ya CCM katika utekelezaji wa ujenzi wa shule za sekondari za kujenga ujuzi lakini pia unatafsiri maono ya Rais Samia katika kuijenga Tanzania yenye wataalam katika kila ngazi hadi ngazi ya vijiji.

Baadhi ya mabalozi wa chama cha mapinduzi waliohudhuria ziara hiyo  ya ukaguzi Juma Spark na Liberata James wamemshukuru Rais Samia kwa ujenzi wa shule hiyo kwani imesogeza karibu elimu ya ujuzi kwa watoto wao ambayo vinginevyo wangeipata mbali na kwa gharama kubwa.

Awali Afisa elimu Sekondari wa Halmashauri ya wilaya Kigoma,Exavery  Ntambala alisemaa kuwa Zaidi ya shilingi Milioni 600 zimetumika kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo na tayari mwaka huu shule hiyo imeanza kuchukua wanafunzi na masomo yameanza.



 

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3