DKT ALBINA CHUWA ATEULIWA MWENYEKITI MPYA YA BODI TAASISI YA KIMATAIFA YA TAKWIMU (ISI)
Feb 4, 2026
Matukio Daima, Morogoro
Tasnia ya takwimu nchini Tanzania imepata heshima kubwa duniani baada ya Dk Albina Andrew Chuwa kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Maadili ya Taasisi ya Kimataifa ya Takwimu (ISI)
Dk Chuwa, aliyewahi kuongoza Ofisi ya Taifa ya Takwimu NBS kwa mafanikio makubwa kwa zaidi ya miaka 17, amepewa jukumu la kusimamia misingi ya uadilifu wa takwimu duniani.
Wadau wa sekta hiyo wamesema uteuzi wake ni matokeo ya kazi kubwa aliyofanya katika kuhakikisha takwimu sahihi na za kuaminika.
Chini ya uongozi wake, bodi hiyo inatarajiwa kuimarisha usalama wa taarifa na matumizi ya data kwa manufaa ya jamii.
Nafasi hiyo awali ilikuwa ikishikiliwa na Prof Walter Josef Radermacher wa nchini Ujerumani ambaye muda wake umemalizika
