Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
MBUNGE JUMAA AFUTURISHA VIONGOZI WA CCM KATA 6 MLANDIZI AWASHUKURU, AOMBA USHIRIKIANO ZAIDI

MBUNGE JUMAA AFUTURISHA VIONGOZI WA CCM KATA 6 MLANDIZI AWASHUKURU, AOMBA USHIRIKIANO ZAIDI

 

Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud Abuu Jumaa amekutana na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi  katika mkutano maalumu wa kutoa shukran  zake za dhati kwao kwa kumchagua kuwaongoza Jimboni humo.


Mhe.Mbunge Hamoud amesema hayo  kwenye  mkutano  uliofanyika Malandizi Stendi, Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani ambao umehudhuriwa na viongozi kutoka kata sita za Mlandizi Mjini.


"Baada ya miezi mitatu kupita ya uchaguzi  leo nimekuja hapa ili niwashkuru kwa kusimama nami kwenyw uchaguzi na kunichagua kuwa mwakilishi wenu kwa mara nyingine tena nasema mimi siyo mjanja sana bali ni Mwenyeezi Mungu Mungu amepanga iwe hivi" amesema Jumaa.


" Nawashukuru sana kwa kunichagua kuwa Mbunge  wenu, Wabunge wawili  wa Viti Maalumu Asha Baraka na Hawa Mchafu  pamoja na Madiwani 14wa kuchaguliwa na wa Viti Maalumu  watano  haya ni mafanikio  makubwa kwa sababu nikiangalia safu yote ni majembe huvyo tupeane muda" amesisitiza Mhe.Jumaa.


Amesema kuwa anawashukuru pia kwa kumchagua Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan pia amewaomba wana CCM  kumpa ushirikiano  Mhe.Rais Dkt Samia  hasa katika kipindi hiki  ambacho  anakwenda kumalizia ngwe yake ili aweze kutekeleza  mambo mengi makubwa katika nchi  yetu" amesema Mhe. Jumaa.


"Tunatakiwa  wote kwa pamoja tumsaidie Mhe.Rais Dkt. Samia ili tuweze kuifikia Tanzania yenye mafanikio  na kicheko kwa wote" amesema Mhe.Mbunge  Jumaa.


Aidha Mh.Jumaa ameanza kwa kukutana na Kata sita ambazo ni Mlandizi, Mtambani, Kawawa,

Mtongani,Janga na Kilangalanga.


Wakati huohuo ametoa ahadi lukuki ikiwa ni pamoja na kujenga maduka makubwa na ya kisasa Shopping Mall,Machinjio, Shule mpya kata ya Janga, atajenga Zahanati Kata ya Kawawa.


Mhe.Jumaa ameongeza kwa kusema kuwa  wamekusudia  kujenga jengo  la Chama Cha Mapinduzi (CCM)  huku akisisitiza  kwa kusema kuwa Mungu akimjaalia  atajenga kwa fedha zake mwenyewe.


"Baadaye tutapita  katika ofisi zote za  Kata kuangalia changamoto  walizo nazo na tutazitatua .


Akizungumza  kuhusu uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa  utakaofanyika  2027 amewasisitiza  Viongozi wote ambao wanajiona hawana uwezo wa kuongoza wajiengue mapema na kuatafuta warithi wao ikiwa pamoja na kuwaandaa vijana wenye wito  ambao wana uwezona watakaowavusha katika uchaguzi huo ujao.


Katika kikao hicho cha Halmashauri  Kuu Cha Sita  cha Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kibaha Vijijini kimeongizwa na  Mwenyekiti wake  Mkali  Kanusu ambaye amesisitiza  kuwa mwakani atagombea tena katika nafasi hiyo.


"CCM ni Chama kizurikinatulea kinatuheshimisha pia tunadhaminika  hivyo tunendelee kukijenga  kwa makundi kwa maslahi ya Chama chetu hivyo wote kwa sasa tukubaliane  kufanya kazi na kushirikiana  kwa pamoja.


Mimi ndiyo mwakilishi wa Mhe.Rais Dkt Samia hivyo hata kama hunipendi hunitaki  wewe njoo tuzungumze  kwa maslahi ya Chama chetu ili wote kwa pamoja tulete maendeleo. 


"Nimedhamiria kupambana kupandisha  Mamlaka ya Mji ,na jambo linakwenda vizuri katika ngazi za juu ikiwamo Wilaya na Mkoa.


Endapo tutapandishwa hadhi tutapata faida  ya Mji kupangika kisasa ,kupata ongezeko katika ruzuku  barabara  zitajengwa katika kiwango cha lami ,pia ikumbukwe kuwa 2025-26 tumeongoza kwa nchi nzima kwa kukusanya mapato  hili ni jambo la kujivunia ,tutamaliza ujenzi wa soko ,stendi ya mabasi tutajenga hoteli kubwa na ya kisasa maegesho ya magari.


Aidha Mhe.Jumaa amezitaja baadhi ya barabara ambazo ziko katika  mpango wa kujengwa katika kiwango cha lami ni Chalinze Gwata, Utete, Rufiji na Makofia Mlandizi Mzenga.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3