Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
MAJAMBAZI WATATU WAUWAWA WAKIJARIBU KUIBA FEDHA SIMIYU MONEY.

MAJAMBAZI WATATU WAUWAWA WAKIJARIBU KUIBA FEDHA SIMIYU MONEY.

 





Na COSTANTINE MATHIAS, Matukio Daima-Simiyu.

Jeshi la Polisi Mkoani Simiyu kupitia Kikosi Maalumu cha Kuzuia na Kupambana na Uhalifu wamefanikiwa kuuwa watu watatu katika majibizano ya risasi ambao walikuwa wnavunja milango ya jengo la Simiyu Money Service. 

Katika taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoani humo Edith Swebe mbele ya Waandishi na imeelezwa kuwa February 8, majira ya saa 8:30 usiku katika mtaa wa NMB, kata ya Malambo, watu watatu waliuwawa Kwa majibizano ya risasi na askari Polisi. 

Taarifa hiyo imeelezwa kuwa, tukio hilo lilimetokea baada ya Polisi kupokea taarifa kuwa Kuna watu watatu wanavunja milango ya Jengo la Simiyu money services linalotumiwa linalotumiwa kutoa huduma ya miamala ya fedha ya makampuni ya simu na kibenki. 

"Kikosi Maalumu cha Kuzuia na Kupambana na uhalifu walifika katika eneo hilo na Watu waliokuwa wanatekeleza uhalifu katika jengo hilo walipobaini wanafuatiliwa walianza kufyatua risasi jambo ambalo liliwalazimu kujibu mapigo na kufanikiwa kuuwa watuhumiwa watatu" imeeleza sehemu ya taarifa hiyo. 

Imeelezwa kuwa watuhumiwa hao walipoteza maisha wakati wanakimbizwa hospitali Kwa matibabu na kwamba askari walifanikiwa kupata silaha moja aina ya Ak47 waliokuwa wanatumia majambazi hao na risasi nane ndani ya magazini, pia katika upekuzi walikutwa wakiwa na shilingi mia tatu fedha za Kenya, noti ya shilingi 5 ya Misri, tiketi ya kutoka Migori kuja Silari na tiketi za Silari hadi Lamadi. 

Aidha, Jeshi la Polisi Mkoani Simiyu linaendelea na opereshaeni na misako kukabiliana na wachache ambao hawataki kujitafutia kipato kwa njia halali, pia  linawashukuru wananchi kwa ushirikiano wao katika kubaini na kutanzua uhalifu,  na pia linatoa wito kwa baadhi ya watu  wanaoendekeza kufanya uhalifu sababu hasara yake ni kubwa mno. 

Mwisho.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3