Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
MADIWANI BARIADI VIJIJINI WAPITISHA BAJETI YA SHILINGI BIL 39.5.

MADIWANI BARIADI VIJIJINI WAPITISHA BAJETI YA SHILINGI BIL 39.5.

 



Na COSTANTINE MATHIAS, Matukio Daima-Simiyu.


BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, limepitisha Mpango wa Rasimu ya Mapendekezo ya Bajeti ya shilingi Bil. 39.5 kwa mwaka wa fedha 2026/2027.


Mapendekezo ya Bajeti hiyo yanahusisha makusanyo ya fedha za ndani (Own Source), Mishahara na fedha kutoka Serikali Kuu. 



Akizungumza mara baada ya kupitisha Rasimu ya Mapendekezo hayo, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo,  Mayala Lucas amewataka Madiwani wenzake kuwa mstari wa Mbele kusimamia ukusanyaji wa mapato ili waweze kufikia la Bajeti hiyo na kuwaletea wananchi Maendeleo.


Mwenyekiti huyo pia amewataka Mweka hazina na Mwenyekiti wa kikosi cha ukusanyaji mapato kuhakikisha wanasimami la ipasavyo ukusanyaji wa mapato hususani wakati huu wa Biashara ya choroko kwa kuhakikisha kila bajaji inayosafirisha inakatiwa ushuru.


Awali akiwasilisha Umbile la Bajeti hiyo, Afisa Mipango wa Halmashauri hiyo, Sayi Luseba amesema kuwa katika Bajeti ya mwaka wa Fedha 2026/2027, wamependekeza na kukisia kukusanya na kutumia kiasi cha shilingi Bil. 39.5 fedha ambazo zitatokana na makusanyo ya ndani, Mishahara na serikali Kuu. 




Mwisho.








Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3