Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
 MADIWANI BARIADI MJI WAPITISHA BAJETI YA SHILINGI BIL. 36.1

MADIWANI BARIADI MJI WAPITISHA BAJETI YA SHILINGI BIL. 36.1





Na COSTANTINE MATHIAS, Matukio Daima-Simiyu.



BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu, limepitisha Mpango wa Rasimu ya Mapendekezo ya Bajeti kwa mwaka wa fedha 2026/2027 yenye thamani ya shilingi Bil. 36.19 ikiwa ni ongezeko la asilimia 5 .2 ya mwaka wa fedha 2025/2026.


Mapendekezo ya Bajeti hiyo yanahusisha makusanyo ya fedha za ndani (Own Source), Mishahara na fedha kutoka Serikali Kuu. 


Akiwasilisha Bajeti hiyo, Mkuu wa Divisheni ya Mipango na Uratibu, Imelda Kirima amesema Bajeti hiyo imeandaliwa Kwa kuzingatia mahitaji na maslahi ya wananchi wote ukilenga kuboresha Ustawi wa Jamii na kiuchumi. 



Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Nkenyenge Charles amewataka Watendaji kushirikiana na Madiwani katika ukusanyaji wa Mapato ili kufikia malengo ya Bajeti hiyo. 


Diwani wa Kata ya Somanda, Majaba Malase amewataka Watendaji kuongeza umakini kusimamia ukusanyaji wa mapato katika Stendi ya mabasi Somanda ambayo imejengwa na serikali kwa gharama kubwa. 


Mwisho.







Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3