MAAMBUKIZI YA SEHEMU ZA UZAZI (PID) HUWATESA SANA WANAWAKE NA WASICHANA
Na Ester Sebastian (UOI) Matukio Daima Media.
Nesi wa Hospitali ya Aghakani mkoa wa Iringa Sharif Ally ameelezea namna maambukizi ya sehemu za uzazi inavyowasumbua wasichana pamoja na wanawake hupelekea kuwa mgumba.
Amesema kuwa maambukizi ya sehemu za uzazi huwambukiza kwa njia ya kujaamiana kimwili au kutokuwa na usafi kikamilifu yaani kuvaa nguo ya ndani kwa muda mrefu bila kufua au kujamiana na mwanaume tofauti tofauti bila kinga.
"Ugonjwa huu hutesa sana wasichana na wanawake na ukichelewa matibabu wa ugonjwa huu hupelekea kuwa mgumba na ugonjwa huu huambukizwa kwa njia ya kujamiana kimwili na wanaume tofauti tofauti au kutokuwa msafi na nguo za ndani" Alisema Ally.
Mkazi wa Kihesa Mwajuma Kalinga amesema ugonjwa huu ni hatari sana kwa wanawake na kwa wasichana kwasababu kutokwa na harufu mbaya ukeni kutokuwa na amani huwashwa sehemu za siri na hupelekea kuwa mgumba.
"(PID) ni ugonjwa hatari sana kwa wanawake au wasichana hupelekea kupata muwasho sehemu za siri kutokwa na ushafu wenye harufu kali kutojiamini katika kundi la watu na mwisho wa siku kuwa mgumba kabisa" Alisema Kalinga.
Mkazi wa Tumaini Irene Lucky amesema natoa ushauri kwa wanawake au wasichana wote wakapo hisi wanaugonjwa huu wakimbilie vituo vya afya ili waweze kupata matibabu kwa muda sahihi ili kupunguza idadi ya ugumba unao sababishwa na( PID).
"Ili kuepukana na ugonjwa (PID) lazima wanawake na wasichana tuwe macho ukihisi unadalili yoyote kuhusiana na ugonjwa wa (PID) kimbilia kwenye vituo vya afya na usione aibu maana wasichana na wanawake huona aibu kwenda hospitali wakijihisi wana ugonjwa huo" Alisema Lucky.
