FURSA MPYA YATANGAZWA KWA WAONGOZA WATALII
Na;Jusline Marco,Arusha
Uongozi Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro umeibua mabadiliko makubwa katika ushirikiahwaji wa wadau wa sekta ya utalii, ikianza mwanzo wa safari mpya ya simulizi kwa chapa ya Destination Ngorongoro kwa kuzungumza sauti moja, iliyo thabiti, yenye kujiamini na kukumbukwa.
Akitangaza kampeni hiyo Kamishna Msaidizi Mwandamizi anayesimamia huduma za Utalii na Masoko Mariam Kobelo ameeleza kuwa shindano linahusu eneo la Ndutu ambapo ndipo Safari Kuu ya Nyumbu huzaliwa na maisha kuanza, ambapo eneo hilo pia hadithi ya Ngorongoro hujirudia upya kila mwaka.
Ngorongoro imeamua kuzindua shindano la upigaji picha kwa waongoza watalii lijulikanalo kama “The Birth of Wonders photo competition” katika eneo la Ndutu hususan msimu huu wa mazalia ya Nyumbu.
Katika shindano hilo la upigaji picha washindi watachaguliwa kwa kuzingatia ushiriki wa watazamaji pamoja na kufuata masharti yote ya shindano ambapo mshindi wa kwanza atajinyakulia kitita cha shilingi Milioni 3,000,000, mshindi wa pili shilingi milioni 2,000,000 na mshindi wa tatu atajishindia shilingi milioni 1,000,000.
Amebainisha kuwa waongoza Watalii ambao ni washiriki wa kampeni hiyo wanakuwa wasimulizi wa sauti ya chapa ya Destination Ngorongoro kwani wao ndiyo mashuhuda wa kwanza wa simulizi ya uzao wa nyumbu.




