CCM YARIDHISHWA NA SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA MKOA WA KILIMANJARO
CHAMA cha Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro kimeridhishwa na utendaji wa siku 100 za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mkoa huo ambapo ulipokea fedha za maendeleo Bilioni 112.63.
Hayo yamebainishwa na Katibu wa Siasa na Uenezi mkoa wa Kilimanjaro, Ibrahim Urio alipozungumza na waandishi wa habari ambapo alisema kuwa Chama kimeridhishwa na utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ndani ya siku 100.
Amesema kuwa, ndani ya siku hizo mkoa ulipokea fedha za ujenzi wa stendi ya mabasi ya Ngangamfumuni Bilioni 19.7, kuanza kwa ujenzi wa stendi ya mabasi halmashauri ya wilaya ya Mwanga Bilioni 3.8 na Bilioni 33.33 kwa ajili ya kupeleka umeme kwe
"Ndani ya siku 100 kumeanza ujenzi wa soko la kisasa la Kwa sadala wilayani Hai wenye thamani ya Bilioni 11.6, pia kuanza kwa ujenzi wa mradi wa Bwawa la Yongoma wilayani Same wenye thamani ya Bilioni 44.2" Amesema Urio.
Ameongeza kuwa, katika kipindi hicho pia mkoa umepokea Watumishi wapya wa kada mbalimbali 1914 wakiwemo sekta ya afya 273, sekta ya elimu 372 na kada zingine Watumishi 1269.
