Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
BAJAJI ZA MIKATABA ZINA FAIDA PAMOJA NA CHANGAMOTO

BAJAJI ZA MIKATABA ZINA FAIDA PAMOJA NA CHANGAMOTO

 

Na Ester Sebastian – Matukio Daima Media (UoI)

Madereva wa bajaji Mjini Iringa  mkoani Iringa  wameeleza faida na changamoto za mfumo wa kumiliki vyombo hivyo kwa njia ya mikataba, wakibainisha kuwa mikataba hiyo imegawanyika katika makundi mawili makuu; mkataba wa benki na mkataba wa mtu binafsi.

Akizungumza na Matukio Daima Media , dereva wa bajaji Israel Gadau alisema mkataba wa mtu binafsi una faida ya kumwezesha dereva kumiliki chombo chake mara baada ya kumaliza muda wa makubaliano.

“Faida ya mkataba wa mtu binafsi ni kwamba ukimaliza muda mliokubaliana na mmiliki, bajaji inakuwa yako. Hata hivyo, changamoto yake ni kukosekana kwa utaratibu rasmi wa kisheria, hali inayoweza kusababisha migogoro endapo mmoja atakiuka makubaliano,” alisema Gadau.

Kwa upande wake, dereva wa eneo la Kihesa, Ismail Tinyi, alisema mkataba wa benki una uhakika zaidi kisheria na humwezesha dereva kumiliki chombo baada ya kumaliza malipo yote kwa wakati.

“Faida ya mkataba wa benki ni kwamba ukikamilisha malipo kama ilivyokubaliwa, chombo kinakuwa chako rasmi. Changamoto yake ni gharama kubwa ya malipo ya awali, jambo linalowafanya madereva wengi kushindwa kujiunga na mfumo huo,” alisema Tinyi.


Naye dereva mwingine wa Kihesa, Kennes James, aliiomba serikali kuangalia upya vigezo vya utoaji wa mikopo au mikataba ya benki ili viwe rafiki kwa madereva wengi zaidi.

“Tunaomba serikali ipunguze masharti na vigezo vya mikataba ya benki ili madereva wengi waweze kumiliki vyombo vyao kupitia taasisi rasmi badala ya kutegemea mikataba ya mtu binafsi,” alisema James.

Kwa ujumla, madereva hao walisema kuwa licha ya changamoto zilizopo, mfumo wa mikataba umechangia kuwainua kiuchumi baadhi yao kwa kuwapa fursa ya kumiliki bajaji na kuboresha maisha yao. kuwa   kuwepo kwa mikataba iliyo rasmi na inayolindwa kisheria ili kuepusha migogoro na kulinda maslahi ya pande zote.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3