Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
TRA KIGOMA YAGUSA MAISHA YA WATOTO WENYE MAHITAJI

TRA KIGOMA YAGUSA MAISHA YA WATOTO WENYE MAHITAJI

 

Meneja Msaidizi huduma kwa mlipa kodi (TRA) mkoa Kigoma,Kwizera Ntibakazi (kushoto) akikabidhi misaada mbalimbali kwa uongozi na   wanafunzi wenye mahitaji wa Shule ya Msingi Maalum Kabanga iliyopo wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma ambapo TRA imekabidhi vitu mbalimbali ikiwemo vyakula, magodoro na vifaa vya elimu vyenye thamani ya shilingi milioni nane.


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

MAMLAKA ya mapato (TRA) mkoa Kigoma imetoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo vifaa vya shule, chakula na magodoro kwa shule Msingi Maalum Kabanga wilayani Kasulu mkoani Kigoma ikiwa ni kurudisha shukrani kwa walipa kodi wake.

Msaada huo wenye thamani ya shilingi Milioni nane ulikabidhiwa kwa uongozi wa shule hiyo ya wanafunzi wenye mahitaji na Meneja Msaidizi huduma kwa mlipa kodi (TRA) mkoa Kigoma,Kwizera Ntibakazi kwa niaba ya Meneja wa mkoa Kigoma, Beatus Nchota.


Akizungumza wakati akikabidhi msaada huo Kwizera aliitaja misaada hiyo kuwa ni pamoja na maharage, mchele, sukari, sabuni pamoja na mahitaji mengine ya msingi ikiwemo mabegi ya kuwekea madaftari kwa wanafunzi na magodoro ya kulalia wanafunzi.

Kwizera alisema kuwa msaada huo ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa uwajibikaji wa kijamii wa taasisi (Corporate Social Responsibility) na mchango wake katika kuboresha ustawi wa makundi yenye uhitaji maalumu.

Kwa upande wake Mwalim Mkuu wa shule hiyo ya Msingi Kabanda Maalum, Kulwa Godlucky ambaye alisema kuwa shule hiyo ina watoto 141 wenye mahitaji maalum na serikali imekuwa ikisaidia kuendesha shule hiyo lakini bado mahitaji mbalimbali kwa watoto hao yamejitokeza na hivyo kutolewa kwa misaada kama hiyo kunasaidia kukabili changamoto inayojitokeza.

Mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo Timotheo Mapengo mwanafunzi wa darasa la sita ameishukuru TRA kwa msaada huo kwani misaada hiyo imekuwa  ikikabili changamoto walizonazo ambazo nyingine wazazi wao wanashindwa kuwanunulia hivyo wadau wamekuwa msaada kwa hilo.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3