MAWAKILI WA SERIKALI KUENDESHA KLINIKI YA HUDUMA ZA KISHERIA SIMIYU.
Na COSTANTINE MATHIAS, Simiyu.
JOPO la Mawakili wa serikali linatarajia kuzindua Kliniki ya huduma za kisheria kwa wananchi katika Mkoa wa Simiyu, ambayo itatolewa bure kwa muda wa siku saba ili kutatua migogoro inayowakabili wannachi.
Aidha, imeelezwa kuwa Huduma hizo pia zitapungua malalamiko ya kisheria kutoka kwa wananchi na kuchochea masuala ya Uwekezaji ili kunufaisha wananchi na Maendeleo kwa ujumla.
Hayo yamebainishwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, AnaMringi Macha wakati akiongea na waandishi wa Habari ofisini kwake ambapo alisema watazindua Kamati za kisheria ngazi ya Mkoa na wilaya ili kushughulikia masuala ya kisheria.
Alisema kuwa Kliniki ya kisheria itafanyika Kwa siku nane na Uzinduzi wa Kamati ya kisheria ngazi ya Mkoa wa Simiyu, utazinduliwa tarehe 3.2.2026 na kuhitimishwa tarehe 8.2.2026 katika uwanja wa CCM mjini Bariadi ambapo Kamati hizo zitakuwa za kidumu na zitashukughulikia masuala ya kisheria kutokana na ubobezi wa Wanasheria hao.
Alisema kuwa Kamati hizo zitatoa Elimu ya Sheria kwa umma katika kushughulikia changamoto katika maeneo mbalimbali ikiwemo Mashauri ya ndoa, mirathi na ardhi ambayo hayaleti utengamano katika jamii.
Macha alileza kuwa Kamati hizo zitapunguza masuala ya migogoro dhidi ya serikali na Wananchi ili kuwewawezesha wananchi kupata muda wa kusikilizwa na kupata haki zao.
Alisema kwamba Kamati hizo zitatoa huduma ya Ushauri wa kisheria kwa kukutanisha mawakili wa serikali, mawakili wa Taasisi mbalimbali na Wananchi wenye changamoto mbalimbali ili kutatuliwa migogoro yao
Alisisitiza kuwa Uwepo wa huduma hizi utawezesha mawakili kusimamia Utawala wa sheria katika maeneo ya Mkoa wa Simiyu na Kamati hizo zitawezesha mawakili kushirikiana na Wadau wengine wakiwemo Mawakili wa kujitegemea katika kutatua kero za Wananchi.
"Tunampongeza Rais Dk. Samia kwa kulinda haki, kukuza demokrasia, kutetea haki za Wananchi, kupinga Vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu, amesimamia misingi ya Utawala Bora, na kupinga ukatili wa kijinsia na ameheshimu Utawala Bora" alisema Macha.
Kwa upande wake, Wakili wa serikali mwandamizi, kutoka ofisi ya mwanasheria Mkuu wa serikali, Silinde Gumada alisema kuwa maelengo ya Kamati hizi ni kusikiliza migogoro ya wananchi dhidi ya serikali kabla mwananchi hajaipeleka serikali Mahakamani.
Alisema kuwa Kamati hizo zitashauri pia wananchi juu ya migogoro ya mirathi, ndoa na ardhi ili waweze kupata Elimu ya Sheria na kuleta utengamano wa kijamii huku akiwataka wananchi kuchangamkia fursa hiyo.
Alifafanua kuwa kliniki hizo zitawasaidia wananchi kuandika wosia na pia kushughulikia malalamiko mbalimbali ya wananchi ili yaweze kutatuliwa na Kwamba Kamati hizo zitakuwa endelevu na kusimamia na Mkuu wa Mkoa kwa ngazi ya Mkoa pamoja na Wakuu wa Wilaya ngazi ya wilaya.
Wakili Gumada alisema kuwa kila wilaya ya Mkoa wa Simiyu, klikini hizo zitawafikia wananchi katika maeneo yao mpaka ngazi ya kata pia kutakuwepo na mawasiliano ili kurahisisha utoaji wa huduma ya kiliniki za kutatua migogoro ya kisheria.
Wakili wa serikali mwandamizi, kutoka ofisi ya mwanasheria Mkuu wa serikaliakili Gumada akizungumzia Utekelezaji wa kliniki ya kisheria na namna ambavyo watahudumia wananchi na kutatua migogoro bila malipo.Aliongeza kuwa katika timu ya Mawakili, watakuwepo wataalamu wa sheria kulingana na tatizo la mwananchi ikiwemo migogoro ya ardhi, ndoa, mirathi na kwamba jopo hilo lina wataalamu waliobobea katika Sheria.
XxxxX




