Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
WAZIRI SIMBACHAWENE AWAPONGEZA ASKARI KWA KUHAKIKISHA AMANI INATAWALA.

WAZIRI SIMBACHAWENE AWAPONGEZA ASKARI KWA KUHAKIKISHA AMANI INATAWALA.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, ametoa pongezi kwa Askari wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama kwa kuhakikisha hali ya amani na utulivu inaendelea kudumishwa nchini, licha ya kuwapo kwa taarifa za fununu za maandamano yasiyo na kikomo yaliyodaiwa kupanga kutekelezwa katika maeneo mbalimbali.

Akizungumza baada ya kukutana na Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) pamoja na Askari wa Jeshi la Polisi waliokuwa doria katika mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam, Simbachawene alisema vikosi hivyo vimeendelea kutimiza wajibu wao kwa weledi na uzalendo wa hali ya juu.


Waziri huyo alibainisha kuwa uwepo wa askari barabarani umeongeza kujiamini kwa wananchi na kudhibiti taarifa potofu zilizoenezwa kuhusu uwezekano wa machafuko, akisisitiza kuwa Serikali haitasita kuchukua hatua dhidi ya watu wanaojaribu kuhatarisha amani ya nchi.


Aliongeza kuwa Wizara yake itaendelea kuimarisha ushirikiano kati ya vyombo vya ulinzi na usalama ili kuhakikisha Tanzania inaendelea kuwa nchi salama kwa wananchi na wageni.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3