HEART TO HEART NA KOIKA WAKABIDHI VISIMA VITANO HALMASHAURI YA MTAMA
KATIKA kuunga mkono jitihada za Serikali Katika kutatua tatizo la Maji Taasisi ya Heart to heart Foundation kwa kushirikiana na KOICA imekabidhi visima vitano vyenyewe thamani ya milioni 110 Katika halmashauri ya Mtama Mkoani Lindi
Akizungumza Katika ghafla ya makabidhiano ya visima hivyo iliyofanyika Katika kijiji cha Mtegu huko Halmashauri ya Mtama mwishoni mwa wiki iliyopita Meneja Mradi wa heart to heart Foundation Deodatus Manzi Amesema kuwa visima hivyo ni sehemu ya Utekelezaji wa Mradi wa miaka 3 wa maji Safi na usafi wa mazingira ambao unalenga kufikia Kata 14
Alisema Katika awamu ya Kwanza ya Utekelezaji wa Mradi huo utajikita Katika kusambaza miundombinu ya maji Katika zahanati na vituo vya Afya ambapo mpaka sasa tayari visima 11 vimeshachimbwa
"Mwaka Jana tulichimba visima sita na sasa hivi vitano Jumla nitakuwa 11 hivyo tukio la Leo nisehemu ya kuweza kukabidhi Miradi hiyo"
Kaimu mkurugenzi wa halmashauri hiyo ya Mtama Tasilo Lupapa alisema kupitia Mradi huo Jumla ya wananchi 2987 kutoka Katika Vijiji vya Simama, Ingawali , Mbawala, Litipu na Mtegu watanufaika
Adha Lupapa licha ya kuwashukuru heart to heart kwa msaada huo pia alitoa wito kwa wananchi na jumuoya za watumia maji kuilinda miundo mbinu hiyo ili itumike kwa muda mrefu
" Ni matumaini yangu kuwa kamati za maji zilizopo kamati za usimamizi wa vituo na viongozi na wananchi wote tutashiriki Katika kutunza miundombinu hii ili iweze kudumu na kuleta manufaa yaliyokusudiwa kwa Jamii yote"
Alisema itakuwa ni jambo la kushangaza kuona Miradi hiyo inakwama kiuendelevu na uendeshaji muda mfupi baada ya kukabidhiwa Katika vijiji hivyo.
Mganga mfawidhi wa zahanati ya mtegu Dr. Jacklin Sitta Alisema kuwa kwa kusogezewa huduma ya maji Katika zahanati hiyo kutarahisisha utosji na upatikanaji wa huduma Kwa wagonjwa wanaokuja kupata huduma.
" Kwa sasa hapa Katika zahanati yetu tunatuma maji ya mvua ambayo tunayakinga ama kuyahifadhi kipindi cha masikaa ila changamoto kubwa ni pale ambapo maji hayo yakiisha inatulazimu kuyafanya umbali wa km 1 ili kufua huduma hiyo
Baadhi ya wananchi wa Mtegu akiwemo ghalia Saidi na Asha swalehe walisema kuwa kwa sasa inapotokea unampeleka mama mjamzito wakati ambao maji yameisha hospialini hapo ulazimika kubeba maji majumbani kwao yatakayowawezesha kuendelea kupata huduma
" Yani kiukweli tunashukuru kupata maji hapa kwenye Zahanati yetu maana kuna wakati tunalazimika kuja na maji kutoka nyumbani kutokana na uhaba uliokuwepo hapa zahanati ila baada ya kuja huu Mradi kwa kweli tunashukuru utatusaidia wananchi hasa Sisi akina Mama tunapokuja kujifungua " Alisema Bi.Aisha Swalehe



