WORLD TRAVEL AWARDS GRAND FINAL 2026 KUFANYIKA NDANI YA HIFADHI YA SERENGETI 12 DECEMBER
Nov 6, 2026
Tanzania inaenda kuandika historia kubwa duniani kwa kuandaa Fainali kuu ya World Travel Awards 2026, tarehe 12 Desemba ndani ya Four Seasons Safari Lodge Serengeti, katikati ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Hayo yamebainishwa mjini London 5 November katika maonesho makubwa ya utalii duniani ya World Travel Market, Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Ashatu Kijaji pamoja na Mwanzilishi wa World Travel Awards, Graham Cooke, na kuitangaza Tanzania kama mwandaaji.
Hii ni mara ya kwanza katika miaka 33 ya WTA kwa tukio kubwa kama hili kufanyika katikati ya pori, na ni heshima kubwa kwa Tanzania kwa sababu itawakaribisha viongozi wakubwa wa utalii duniani na kuwaonyesha vivutio vyetu vingi nchini ikiwemo Hifadhi ya Serengeti na Ngorongoro hadi Zanzibar na Mlima Kilimanjaro na vingine vingi.
World Travel Awards iliyoanzishwa mwaka 1993 ndiyo tuzo kubwa zaidi za utalii duniani, na fainali yake hukutanisha washindi bora kutoka kila kona ya dunia.
Na sasa macho yote yanaelekea Tanzania kwa siku hiyo ya Desemba 12 ambayo itakuwa jukwaa la kuonyesha uzuri, ukarimu na utamaduni wetu kwa dunia nzima.
WTA ni kama Oscars za utalii duniani, kwa hiyo dunia yote itaelekeza macho yake Serengeti kwenye usiku huo wa tuzo.
Mwisho.


