Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
WAZIRI WA ULINZI AKUTANA NA JENERALI WA KWANZA MWANAMKE AFRIKA MASHARIKI

WAZIRI WA ULINZI AKUTANA NA JENERALI WA KWANZA MWANAMKE AFRIKA MASHARIKI

 



Na Matukio Daima Media Dodoma


WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Mheshimiwa Dkt. Rhimo Nyansaho (Mb), tarehe 16 Novemba 2026, amemtembelea na kufanya mazungumzo na Meja Jenerali Mstaafu Zawadi Madawili katika makazi yake yaliyopo Upanga, jijini Dar es Salaam.


Meja Jenerali Mstaafu Zawadi Madawili ana historia ya kipekee katika tasnia ya ulinzi na usalama, akiwa mwanamke wa kwanza katika Afrika Mashariki kufikia cheo cha Meja Jenerali, hatua inayodhihirisha mchango wake mkubwa katika utumishi wa kijeshi na ulinzi wa Taifa.


Mazungumzo baina ya Waziri Dkt. Nyansaho na Meja Jenerali Mstaafu Madawili yalilenga kumjulia hali pamoja na kubadilishana uzoefu kuhusu safari yake ya utumishi wa kijeshi, mafanikio aliyoyapata na mchango wake katika kulinda na kuitumikia nchi.


Aidha, ziara hiyo imetoa fursa ya kutambua na kuthamini mchango wa Meja Jenerali Mstaafu Madawili katika historia ya Jeshi na nafasi yake kama mfano wa kuigwa kwa wanawake katika utumishi wa kijeshi na uongozi.



Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3