Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
TOSCI YATAMBULISHA STIKA ZA MICHE BORA YA PARACHICHI HORTI LOGISTICA AFRICA

TOSCI YATAMBULISHA STIKA ZA MICHE BORA YA PARACHICHI HORTI LOGISTICA AFRICA


Yahimiza wanunuzi kuzingatia nembo ya taasisi hiyo kuthibitisha ubora wa miche


Taasisi ya Kudhibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) imewataka wanunuzi wa miche ya parachichi kuhakikisha wanapata miche yenye nembo ya taasisi hiyo ili kuthibitisha ubora wake na kuepuka kununua miche isiyokidhi viwango.

Akizungumza na waandishi wa habari katika banda la TOSCI wakati wa maonesho ya jukwaa la kwanza la HortiLogistica Africa lililofanyika jijini Arusha, Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo, Nyasebwa Chimagu, amesema TOSCI imeanzisha matumizi ya stika maalum kwenye miche ya mbegu za mazao ya bustani, hatua inayolenga kuimarisha udhibiti wa ubora na kuwahakikishia wakulima upatikanaji wa miche bora.

Amesema hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za taasisi hiyo kuhakikisha wakulima wanatumia miche yenye ubora unaokidhi viwango, ili kuongeza tija katika uzalishaji na kuimarisha ushindani wa mazao ya horticulture katika masoko ya ndani na kimataifa.

Aidha, Nyasebwa amewahimiza wadau wa sekta ya horticulture kutembelea banda la TOSCI ili kupata elimu kuhusu ubora wa mbegu na miche ya mazao mbalimbali ya bustani, pamoja na kufahamu aina za mbegu zinazohitajika katika masoko ya kimataifa.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3