Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
RAIS SAMIA AANZA ZIARA YA SIKU MBILI UGANDA

RAIS SAMIA AANZA ZIARA YA SIKU MBILI UGANDA

 

Rais Samia Suluhu na Rais Yoweri Museveni

Rais wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan, ameanza ziara yake ya siku mbili nchini Uganda.

Rais Samia aliwasili mapema leo katika ikulu ya Entebbe na kukutana na mwenyeji wake, Rais Yoweri Kaguta Museveni.

Viongozi hao wanatarajiwa kujadiliana kuhusu nishati, biashara, kilimo,viwanda na jinsi ya kuendeleza ujenzi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP).

Ziara hiyo ya Rais Samia, inafuatia safari ya Rais Museveni ya mwezi Agosti 2026, jijini Dar es Salaam, ambapo viongozi hao wawili walitia saini makubaliano ya kuanzisha kituo cha kikanda cha nishati mkoani Tanga.

Kituo hicho kinatarajiwa kuhifadhi mafuta, kusafisha mafuta ghafi na kuyasambaza.

Kituo hicho kinajengwa kupitia mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), lenye urefu wa kilomita 1,443, litakalo safirisha mafuta ghafi ya Uganda kutoka Hoima hadi pwani ya Tanzania karibu na bandari ya Tanga.

Tazama kwa picha Rais Samia alivyowasili Entebbe:






Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3