MOTO WATEKETEZA HOTEL 6 KWA MPIGO ZANZIBAR
Hoteli sita zilizopo eneo la Nungwi, Wilaya ya Kaskazini A, Unguja, zimekumbwa na janga la moto uliosababisha uharibifu mkubwa wa mali katika baadhi ya maeneo ya hoteli hizo.
Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini A, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo, Mhe; Riziki Daniel Yussuf, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, akieleza kuwa moto huo ulianza mapema majira ya mchana.
Amesema licha ya ukubwa wa tukio hilo, vikosi vya Zimamoto na Uokoaji vimefanikiwa kuudhibiti moto huo, huku chanzo chake kikiwa bado hakijafahamika.
Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya amebainisha kuwa hadi sasa hakuna taarifa za madhara yoyote kwa binadamu yaliyosababishwa na tukio hilo.
TAZAMA MOTO UKITEKETEZA HOTEL 6 ZANZIBAR BOFYA HAPA
Miongoni mwa hoteli zilizopata athari za moto huo ni Makofi, Z Hotel, Nungwi Inn na Baobab, huku hoteli nyingine mbili zikiwa bado hazijafahamika majina yake.
Wakati huo huo, Kamisheni ya Utalii Zanzibar imetoa taarifa kwa wadau wa sekta ya utalii katika eneo la Nungwi, ikiwataka wamiliki wa hoteli, mameneja na waendeshaji wa shughuli za utalii kuchukua tahadhari za kiusalama kwa kulinda mali, wafanyakazi na wageni waliopo katika maeneo yao.
Kamisheni hiyo pia imezitaka hoteli kuhakikisha vifaa vya kuzimia moto vinapatikana na vinafanya kazi ipasavyo, huku ikiagiza wageni walioathirika na tukio hilo kuhamishiwa katika Shule ya Msingi Mkokotoni, ambako taarifa zao zitakusanywa na Kamisheni hiyo na kupangiwa malazi ya muda.KALDAN PRE&PRIMARY SCHOOL IRINGA
Kamisheni hiyo imeeleza kuwa hatua hizo zinalenga kuhakikisha usalama na ustawi wa wageni pamoja na wadau wengine wa utalii wakati hatua za kukabiliana na athari za tukio hilo zikiendelea.