Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
MANISPAA KIGOMA UJIJI  KUJENGA  VYOO VYA KISASA  SHULE ZA MSINGI

MANISPAA KIGOMA UJIJI KUJENGA VYOO VYA KISASA SHULE ZA MSINGI


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

HALMASHAURI ya manispaa ya Kigoma Ujiji imetangaza mpango wa ujenzi  wa vyombo bora katika shule za msingi na maeneo ya umma ikiwa ni kuondoa vyoo vya shimo katika manispaa hiyo.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya mansipaa ya Kigoma Ujiji, Juma  Hamsini alisema hayo katika kikao cha kawaida cha baraza la madiwani ikiwa ni kikao chake cha kwanza tangu ateuilwe kuwa Mkurugenzi wa manispaa hiyo na kubainisha kuwa wilaya hiyo kwa sasa ni wilaya ya mjini hivyo haina maana kwa shule za manispaa hiyo kuwa na vyoo vya shimo.

Sambamba na hilo Mkurugenzi huyo alisema kuwa anakusudia kuwepo kwa vyoo bora katika maeneo yote ya umma ili watu waweze kujisitiri badala ya kwenda kutafuta huduma hiyo kwenye mabaa na kuomba madiwani kumuunga mkono katika kutekeleza mipango hiyo.

Akizungumza katika kikao hicho cha baraza Meya wa manispaa ya Kigoma Ujiji, Mussa Maulid amemkaribisha rasmi Mkurugenzi huyo na kuahidi kwa niaba ya madiwani kushirikiana naye kwa karibu katika kuibua, kutekeleza miradi na kusimamia mapato na matumizi ya halmashauri hiyo kwa manufaa ya wananchi wa halmashauri hiyo huku akiwataka wataalam wa halmashauri hiyo kuwahi kazini na kumpa ushirikiano mkurugenzi aweke kutekeleza majukumu yake

Kwa upande wake Katibu wa CCM wilaya ya Kigoma Mjini, Sadick Kaduro alimkaribisha Mkurugenzi huyo katika halmashauri hiyo ya Kigoma Ujiji na kumweleza kuwa viongozi na wananchi wanapenda kupata maelezo na ufafanuzi wa mambo mbalimbali wanayotaka kusikia hivyo asiogope kuulizwa na badala yake ajitahidi kutafuta majibu kwa mambo yote ambayo viongozi na wananchi wanataka kujua.

Mwisho.




 

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3