JUA LAZUNGUKWA NA UPINDE IRINGA
Nov 16, 2026
Wakazi wa Mji wa Iringa leo wamejionea tukio la kuvutia angani, baada ya jua kuzungukwa na duara lenye rangi zinazofanana na upinde wa mvua, linalojulikana kitaalamu kama “Halo ya Jua” au 22-degree Solar Halo
Tukio hilo limetokea majira ya saa 6:24 mchana na kudumu kwa zaidi ya dakika 22 hivi.
Tukio hilo la kimaumbile hutokea pale mwanga wa jua unapopita kwenye fuwele za barafu zilizoko katika mawingu ya juu aina ya cirrostratus, na kusababisha miale hiyo kupinda na kuunda duara lenye rangi nyingi kuzunguka jua.TAZAMA ILIVYOTOKEA BOFYA LINK HII
Kwa mujibu wa wataalamu wa hali ya hewa, uwepo wa halo ya jua mara nyingi ni ishara ya mabadiliko ya hali ya hewa, hasa kuashiria uwezekano wa kuongezeka kwa unyevunyevu angani au mvua katika siku chache zijazo
