Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
WATAKIWA KUTUMIA MAMLAKA YA MKEMIA KWA MAFANIKIO YA KAZI ZAO

WATAKIWA KUTUMIA MAMLAKA YA MKEMIA KWA MAFANIKIO YA KAZI ZAO



Wadau wa sekta ya Madini, Tiba Asili na Mbadala wametakiwa kutumia Mamlaka ya Mkemia Mkuu wa Serikali ili kuwezesha usalama na mafanikio katika kazi zao wanazofanya.

Wito huo umetolewa leo kwenye kwenye Maonesho ya Tisa Kitaifa ya Teknolojia ya Madini Mkoani Geita na Meneja Mkuu wa Mamlaka ya Maabara ya Serikali Kanda ya Ziwa John Wanjala.

Alisema kuna umuhimu mkubwa wa kufanya uchunguzi wa shughuli hizo ili ziweze kuleta matokeo chanya kwenye jamii kwani madhara yanayoweza kuletelezwa na sekta hizo yaweza kuwa mabaya kwa wananchi.

Wanjala alisema Mamlaka hiyo inavyo vifaa vya kisasa kuwezesha ufanyaji wa utafiti wenye tija kwa sekta hizo zenye mchango katika kukuzanuchumi wa taifa.

Alisema mojawapo ya majukumu yao ni kutoa elimu kuhusiana na namna ya kuweza kufanya shughuli za uchenjuaji wa madini kwa kutumia kemikali bila ya kuleta madhara ya kimazingira na kwa afya ya binadamu.

"Kunapokuwa na uelewa ndani ya jamii juu ya kutumia mamlaka ya Mkemia Mkuu wa Serikali huwezesha wadau kwenye sekta hiyo kuepuka hasara katika kazi zao" alisema Wanjala.

Wajala alisema kupitia uchunguzi wanaofanya wanawezesha wachimbaji kufahamu juu ya uwepo wa madini hivyo wadau hao kuwa na uhakika wa shughuli wanazofanya katika maeneo yao.

Alisema vilevile mamlaka hiyo inalo jukumu la kusimamia mchakato wa sheria zinazoendesha matumizi ya kemikali katika shughuli wanazofanya wadau wa sekta hizo hapa nchini.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3