Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
NAIBU WAZIRI WA MAJI AAGIZA MRADI WA MAJI WA MIJI 28 KAYANGA UANZE  KUTOA HUDUMA DESEMBA 31.

NAIBU WAZIRI WA MAJI AAGIZA MRADI WA MAJI WA MIJI 28 KAYANGA UANZE KUTOA HUDUMA DESEMBA 31.


 Na Matukio Daima News

Kagera,Karagwe.

Naibu Waziri wa Maji Mhe. Mhandisi Kundo Andrea Mathew (Mb)  amemtaka Mkandarasi kuhakikisha kufikia Desemba, 2026 mradi huu uwe umeanza kutoa huduma. 

Hayo ameyasema alipokuwa kwenye Ziara yake Mkoani Kagera akikagua utekelezaji wa maendeleo ya mradi wa Miji 28 uliopo Wilayani,Karagwe, Mkoani Kagera.

"Wananchi wanachohitaji siyo kuona michakato hii wananchi wanahitaji kuona huduma ya maji imefika"

Akiwasilisha taarifa ya mradi huu Mhandisi Daudi Beyanga amesema kuwa 
Mradi huu, umefikia asilimia 79 ya utekelezaji na unatarajiwa kuwanufaisha wakazi zaidi ya 352,790 katika kata 12 na vijiji 34 vya wilaya ya Karagwe. 

Mradi huu unatekelezwa na kampuni ya M/s Afcons Infrastructure Limited na Vijeta Projects and Infrastructures Limited (JV), chini ya usimamizi wa mshauri elekezi WAPCOS Limited.

Mradi unagharimu jumla ya shilingi Bilioni 64.32 za Kitanzania, ukiwa na lengo la kuboresha huduma ya maji safi na salama kwa wakazi wa Kayanga na maeneo mengine Wilayani Karagwe.




 

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3