Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
BABA LEVO AMWAGA MILIONI 30 JIMBO CUP  KIGOMA

BABA LEVO AMWAGA MILIONI 30 JIMBO CUP KIGOMA

 

Na Fadhili Abdallah,Kigoma


KIASI cha shilingi milioni 30 kimetolewa kama zawadi kwa timu  zinazoshiriki mashindano ya mpira wa mpira miguu katika jimbo la Kigoma mjini maarufu jimbo Cup yanayosimamiwa na Mbunge wa jimbo la Kigoma Mjini Clayton Revocatus maarufu Babab Levo.


Akizungumza na waandishi wa habari mjini Kigoma Baba Levo alisema kuwa mashindano hayo ambayo yanatarajia kuanza Oktoba 18 mwaka huu yatashirikisha jumla ya timu 32 kutoka kata 19 za jimbo hilo mashindano yatakayofanyika kwwenye uwanja wa Mwanga Community Centre.


Baba Levo alisema kuwa katika mashindano hayo mshindi wa kwanza ataondoka na fedha taslim kiasi cha shilingi milioni 15, msindi wa pili ataondoka na shilingi milioni 10 ambapo mshindi wa tatu ataondoka na shilingi milioni tano.


Sambamba na zawadi za fedha taslim Mbunge huyo wa jimbo la Kigoma Mjini alisema kuwa pia timu zote 32 zinazoshiriki mashindano hayo zitapewa seti ya jezi na mipira.


Aidha baada ya mashindano hayo ya timu za mtaani Baba Laevo alisema kuwa atageuka mashindano ya shule ambapo shule za msingi na sekondari katika jimbo hilo zitashindana na zawadi nono itatolewa ambapo itatangazwa muda ukifika.



Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3