Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
MTOTO RIDHIWANI AFARIKI, 40 WALAZWA HOSPITALI KWA KULA KANDE, KUNYWA TOGWA-SINGIDA

MTOTO RIDHIWANI AFARIKI, 40 WALAZWA HOSPITALI KWA KULA KANDE, KUNYWA TOGWA-SINGIDA


MatukioDaima, Singida
Jumatatu, Oktoba 19, 2026

Karamu ya shukrani iliyowakutanisha wananchi baada ya kazi ya kijamii katika Kijiji cha Unyambwa, Manispaa ya Singida, imegeuka kuwa majonzi baada ya mtoto Ridhiwani Ayoub Omari, wa miaka 13 kufariki dunia na watu wengine 40 kulazwa hospitalini kufuatia kula kande na kunywa togwa linalotuhumiwa kuwa na sumu.

Mtoto aliyefariki ni mkazi wa Kijiji na Kata ya Unyambwa, Manispaa ya Singida. Sakata la tukio hilo lilianza Oktoba 17, 2026, baada ya washiriki wa kazi ya kijamii kualikwa na familia moja nanbaadaye kula kande na kunywa togwa kama sehemu ya shukrani kwa kazi waliyoifanya.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Matride Kuyeto,ametoa Taarifa  hiyo Jana October 18 amesema watu wawili wanashikiliwa na polisi kuhusiana na tukio hilo, huku uchunguzi ukiendelea kubaini chanzo cha kuugua kwa waathirika na hatua zaidi za kisheria zitakazochukuliwa.

Kwa mujibu wa Kamanda Kuyeto, baadhi ya washiriki walipokula chakula, walianza kusumbuliwa na maumivu ya tumbo na kesho yake Oktoba 18, Ridhiwani alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Zahanati ya Moyo wa Yesu, huku waathirika wengine 40 wakihamishiwa Hospitali ya Manispaa ya Singida kwa matibabu zaidi.

Amesema hali za wagonjwa zinaendelea vizuri na wanaendelea kupatiwa matibabu hospitalini ya Manispaa ya Singida. Hata hivyo, chanzo cha tatizo hilo bado kinachunguzwa, na tuhuma kwamba chakula na kinywaji hicho vilikuwa na sumu hazijathibitishwa rasmi.

Kamanda Kuyeto amewataka wananchi, hususan waishio vijijini, kuwa watulivu wakati Jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi wa tukio hilo. Wananchi wanahimizwa pia kusubiri taarifa rasmi za mamlaka kuhusu matokeo ya uchunguzi na hatua zitakazochukuliwa.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3