AFRIKA, GHUBA KUKUTANA TANZANIA KUJADILI AJIRA
Na Matukio DaimaMedia
Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa mkutano wa Afrika na nchi za Ghuba utakaofanyika Oktoba 5 na 6 mwaka huu, ukilenga kujadili uhamaji wa wafanyakazi, ajira na mahitaji ya soko la ajira, hasa kwa vijana.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu, amesema mkutano huo unaojulikana kama “Doha Dialogue II”, utawakutanisha nchi za Umoja wa Afrika (AU), Baraza la Ushirikiano la Nchi za Ghuba (GCC), Jordan na Lebanon.
Amesema nchi za GCC zitakazoshiriki ni Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Qatar, Kuwait, Oman na Bahrain, huku Tanzania ikiwa nchi ya pili kuwa mwenyeji wa mkutano huo unaofanyika kila baada ya miaka miwili.
Sangu amesema mkutano huo ni mwendelezo wa mkutano wa kwanza uliofanyika Doha, Qatar, Mei 21 na 22, 2024, ulioshirikisha nchi 43, zikiwemo 25 za Afrika, na ulihitimishwa kwa kupitishwa kwa Azimio la Doha lililoweka msingi wa kuendeleza ushirikiano huo.
Amesema mkutano wa mwaka huu utakuwa wa kwanza kufanyika katika bara la Afrika, huku moja ya ajenda kuu ikiwa ni kuimarisha uhamaji wa wafanyakazi kati ya nchi, makubaliano ya uhamaji, ujuzi wa wafanyakazi na mahitaji ya soko la ajira.
Kwa mujibu wa Sangu, washiriki pia watajadili mifumo ya kuhakikisha uhamaji wa wafanyakazi unakuwa salama na wenye tija, pamoja na namna ya kukabiliana na mabadiliko ya teknolojia na mahitaji mapya ya soko la ajira.
Amesema Tanzania itatumia mkutano huo kuimarisha nafasi yake katika mijadala ya kimataifa kuhusu uhamaji wa wafanyakazi, kubaini fursa za ajira ndani na nje ya nchi, kulinda haki za wafanyakazi na kuimarisha ushirikiano na nchi za Afrika na GCC Plus.
Sangu amesema mkutano huo pia unalenga kubadilisha makubaliano na majadiliano yaliyopo kuwa hatua za vitendo na matokeo yanayopimika, hatua inayotarajiwa kuongeza fursa za ajira kwa Watanzania, hususan vijana.
Amesema Serikali chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan inaamini mkutano huo utaimarisha ushirikiano na washirika wa kimataifa, kuongeza ushindani wa wafanyakazi wa Tanzania katika soko la ajira la kimataifa na kufungua fursa zaidi za ajira kwa Watanzania.
KUPIGA KURA KWA MATUKIO DAIMA TUZO ZA SAMIA KALAMU AWARDS HAPA
MATUKIO DAIMA IMETEULIWA KUSHIRIKI TUZO ZA UMAHIRI WA VYOMBO VYA HABARI NA WANAHABARI TANZANIA TUZO HIZI ZIMETOLEWA NA TCRA NA TAMWA
MAARUFU KWA JINA LA SAMIA KALAMU AWARDS (SKA2026)⬇️⬇️⬇️
1:TUZO YA CHOMBO CHA HABARI -MATUKIO DAIMA MEDIA
PIGA KURA YA CHOMBO MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA
2:TUZO YA JINSIA ,WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM
PIGA KURA YA PILI YA MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA
3:TUZO YA AFYA
PIGA KURA YA TATU YA MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA
4:TUZO YA MPIGA PICHA
PIGA KURA YA TATU YA MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA
AHSANTE KWA KUPIGIA KWA KUENDELEA KUTUPIGIA KURA MATUKIO DAIMA MEDIA ENDELEA KUTUPIGIA KURA KILA BAADA YA SAA 24 HADI SEPT 30 KASI YAKO YA KUPIGA KURA NDIO USHINDI .


