Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
MICHEZO YA MABUNGE YA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KUFANYIKA NOVEMBA ;2026 JIJINI ARUSHA.

MICHEZO YA MABUNGE YA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KUFANYIKA NOVEMBA ;2026 JIJINI ARUSHA.

 

Na,Jusline Marco:Arusha

Maspika wa Bunge kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki  wamekubaliana kuwa michezo  ya Mabunge ya mwaka 2026 kufanyika jijini Arusha mwezi Desemba mwaka huu.

Akizungumza baada ya kikao cha dharura kilichofanyika katika Makao Makuu ya EAC jijini Arusha, Mwenyekiti wa Kikao hicho ambaye ni Spika wa Bunge la Seneti nchini Kenya Amason Jeffah Kingi amesema kikao hicho kimeitishwa mahsusi kwa ajili ya kujadili ajenda moja kuu ya kuamua nchi mwenyeji wa michezo hiyo ya kila mwaka inayowakutanisha wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Amason amesema baada ya mashauriano ya pamoja kati ya viongozi wote walioshiriki, wamekubaliana kwa pamoja kuwa Arusha ndiyo itakuwa mwenyeji wa michezo hiyo, na kuahidi kushirikiana na Sekretarieti ya EAC kuhakikisha maandalizi yanafanyika kwa ufanisi na michezo inafanyika bila changamoto

Aidha amefafanua kuwa kikao hicho cha dharura kilikuwa na ajenda moja pekee, hivyo masuala mengine yaliyojitokeza hayakuweza kujadiliwa kwa mujibu wa taratibu za kisheria zinazosimamia mikutano ya aina hiyo.


Kwa upande wake, Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Daniel Sillo, amesema kuwa Tanzania haitakuwa mwenyeji wa Michezo ya Mabunge ya EAC kwa mwaka huu kutokana na majukumu makubwa ya kitaifa na kimataifa yanayoikabili nchi.


Akizungumza katika kikao hicho kwa njia ya mtandao, Sillo amesema Tanzania imejitoa kuandaa michezo hiyo kwa mwaka huu kutokana na kuwa na matukio makubwa yanayotarajiwa kufanyika nchini, ikiwemo Mkutano wa Mabunge ya Dunia unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu pamoja na mashindano ya urembo wa dunia.


Amesema kutokana na hali hiyo, Tanzania imeona ni vyema kutoa nafasi kwa nchi nyingine kuandaa michezo hiyo, huku ikiendelea kushirikiana na wanachama wengine wa EAC kuhakikisha mafanikio ya mashindano hayo.


Hata hivyo Maspika kutoka nchi za Jumuiya hiyo wamekubaliana kukutana tena mwezi Agosti mwaka huu jijini Arusha ili kupitia maandalizi ya michezo hiyo na kujadili masuala mengine ambayo hayakuweza kuingizwa katika kikao hicho cha sasa kutokana na taratibu za kisheria zinazosimamia mikutano ya dharura.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3