Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
MEYA KIGOMA UJIJI AKEMEA MATAMASHA YA USHOGA.

MEYA KIGOMA UJIJI AKEMEA MATAMASHA YA USHOGA.

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

MANISPAA ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma inaelezwa kukumbwa na vitendo vya ushoga na ulawiti vinavyopelekea kuporomoka kwa maadili na utamduni wa mji huo jambo ambalo Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Mussa Maulid ametaka kukemewa kwa nguvu

Meya Maulid amesema hayo akifunga tamasha la utamaduni la  Ujiji lililofanyika kwenye uwanja wa michezo wa Kawawa Ujiji mjini Kigoma ambapo alisema kuwa watu wote wanapaswa kuwakemea na kuwafichua wale wanaoleta matamasha ya ushoga katika mji wa Ujiji.


Kiongozi huyo alisema kuwa mji huo bila kujali itikadi za dini zao umekuwa na mila na desturi za malezi kwa vijana na maisha kwa jumla ambazo zilizingatia maadili, heshima na utu wa mtu lakini kwa sasa mambo hayo yametiwa doa na tamaduni mbalimbali zinazoingia ikiwemo kuwepo kwa matamasha ya ushoga kama lililofanyika Tamasha la Kitaifa la Ushoga katika mji huo.

Akizungumzia kufanyika kwa tamasha hilo kila mwaka Meya Maulid alisema kuwa ni lazima tamasha hilo liache athari chanya kila mwaka ikiwemo kuacha alama kwa jamii ikiwemo kuchangia shughuli za kijamii kama madawati mashuleni na mahitaji mengine kwa watu wenye mahitaji.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Taasisi ya Ujiji Heritage & Development Organization,  Hassan Kabeke alisema kuwa anaungana na Meya wa manispaa ya Kigoma Ujiji katika kukemea mmomonyoko wa maadili yanayotokea Kigoma Ujiji ikiwemo kuwepo kwa matamasha ya ushoga ambayo siyo mila na tamaduni za watu wa mji huo.

Shekhe Kabeke ambaye ni Shekhe wa mkoa Mwanza alisema kuwa watu wa mji huo wasikubali tabia za watu wanaokuja na fedha na kuwataka kufanya mambo ambayo siyo mila na tamaduni zao kwa maana ya kusimamia maslahi yao hivyo wakatae fedha zinazoletwa zinazolenga kuharibu taswira ya mji huo wa kihistoria.

Mwisho.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3