Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
SABABU ZA AJALI BARABARANI ZATAJWA  IRINGA

SABABU ZA AJALI BARABARANI ZATAJWA IRINGA

 


NA EASTER KAMETA (UoI)

MATUKIO DAIMA (UoI)

Maafisa isafirishaji mkoa wa Iringa wataja baadhi ya njia zitakazo saidia ili kuepusha Wimbi kubwa Ajali  za barabarani 

Matukio daima imezugumza na moja ya maafisa usafilishaji wa vyombo vya moto Given Marcus ameeleza kuwa madereva  wote wanapaswa kuzingatia usalama wa magari yao kabla ya kuanza safari  , amewataka madeleva kuwa makinina kufuata sheria za barabarani.

"Madeleva wote wanapaswa kuzingatia usalama wa magari yao kabla hawajatoka  stendi pia kuzingatia ukaguzi wa magari yao mara kwa mara  pia unahitajika umakini wa hali ya juu  awapo barabarani kwani ankua mebeba roho za watu ,kufuata sheria za barabarani  kama vile zebra na taa za barabara ni muhimu kwani inasaidia kuepusha ajali zisizo za razima."

Kwaupande wake Daudi Sanga meeleza kuwa maegesho ya vyombo vya moto yamekuwa changamoto kubwa kwani baadhi ya watu na kutaja kuwa baadhi ya watu hufanya maegesho katika pembe za barabara pia amewataka madeleca bajaji na bodaboda kufuata sheria.


"Madereva bodaboda na bajaji wanekuwa chachu ya kusababisha ajali kwani wao huwa wana lazimisha kupitasehemu ambayo ni ndogo ,hafuati Sheria kwani wao hupita hata kama taa ziwe hazija ruhusu ambapo hali hii huweza kupelekea ajari kea mtumiaji wa barabara anayetembea kea miguu pia baadhi ya madeleva wamekuwa na tabia ya kuegesha vyombo vyao vya moto barabarani hivyo hupelekea  kutokea kwa ajali"

Frank Mwaibunga ameeleza kuwa Vijana wengi wanaendesha vyombo vya usafiri kwa mihemko na mashindano  huku akutaja kuwa hali hii hutokana na kukosekana kwa elimu  juu ya matumizi ya vyombo vya moto.

" Baadhi ya madeleva hawana elimu ya kutosha juu ya  matumizi sahihi ya vyombo vya moto hivyo hupelekea  wao kutumia vyombo hivyo kwa kasi ya  hali ya juu nakupekekea kutokea kwa ajali barabarani  pia wanao endesha vyombo hivyo wengi wao ni vijana wadogowadogo hivyo huendesha kwa mashindano kutokana  hawana elimu hivyo hua wao ni chanzo cha ajali hizo."

John Mbunda ameeleza kuwa baadhi ya madeleva hutumia vilevi kabla ya safari pia ametaja kuwawengine huendesha vyombo vya moto wakiwa wamechoka na wengine wakiwa na mawazo ambapo si sahihi.

 "Matumizi ya  vilevi kwa baadhi madereva kabla ya kuanza safari huku wakidai kuwa wakifanya hivyo inawasaidia katika kujiamini jambo ambalo si sahihi pia madereva wengine huendesha vyombo vya usafiri wakiwa wamechoka ambapo hali hii huweza kufanya kutokea kwa ajali kutokana kwamba mwili na akili haviko tayari kufanya kazi lakini mtu analazimisha piawengine huendesha magari wakiwa na msongo wa mawazo na kupelekea ajali."


Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3