Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
POLISI WACHUNGUZA MAUAJI YA MCHINA MKURUGENZI WA KIWANDA DAR

POLISI WACHUNGUZA MAUAJI YA MCHINA MKURUGENZI WA KIWANDA DAR

 


Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linaendelea na uchunguzi kuhusu tukio la kuuawa kwa mmiliki wa kiwanda cha kuchakata chuma cha XIL LI, raia wa China aliyefahamika kwa jina la Bhaozang Ge (50). 

Tukio hilo lilitokea Mei 16, 2026 majira ya saa 8:00 usiku katika eneo la Mabibo Ubungo jijini Dar es Salaam, ambapo marehemu anadaiwa kushambuliwa na walinzi binafsi wa kiwanda chake na kupoteza maisha akiwa eneo hilo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Mei 19, 2026 na Kamanda wa Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam, uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea ili kuwabaini na kuwachukulia hatua za kisheria wote waliohusika na tukio hilo. 

Jeshi la Polisi limewahakikishia wananchi kuwa hatua stahiki zitachukuliwa mara baada ya uchunguzi kukamilika.


Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3