Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
 MEYA AFUNGUKA MIPANGO YA KUINUA UCHUMI KIGOMA UJIJI

MEYA AFUNGUKA MIPANGO YA KUINUA UCHUMI KIGOMA UJIJI


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

HALMASHAURI ya manispaa ya Kigoma Ujiji inatarajia kutumia kiasi cha shilingi Bilioni 3.5 kwa ajiili ya ujenzi wa soko la Kisasa katika bandari ndogo ya Kibirizi mjini Kigoma ili kutekeleza kwa vitendo mpango wa serikali wa kuufanya mkoa Kigoma kuwa mkoa wa kimkaka kwa uchumi na bishara.

Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Mussa Maulid alisema hayo akizungumza kweny mkutano wa hadhara ulioitishwa na diwani wa kata ya Kitongoni manispaa ya Kigoma Ujiji, Himid Omari akieleza utekelezaji wa mipango mbalimbali ya manispaa katika robo ya tatu ya mwaka huu wa fedha.

Maulid alisema kuwa utekelezaji wa mpango huo utaanza mapema mwezi wa saba mwaka huu kuelekea mwaka wa fedha 2026/2027 ambapo soko hilo litakapokamilika litaweza kuchukua wafanyabiashara 500 kwa wakati mmoja.

Akizungumza katika mkutano huo Diwani wa kata ya Kitongoni manispaa ya Kigoma Ujiji, Himid Omari Mkunda alisema kuwa kupitia baraza la madiwani la halmashauri hiyo wamekubaliana kuhuisha miradi mbalimbali ya maendeleo katika tarafa ya Kigoma Kusini inayojumuishi kata mbalimbali za Ujiji ili kuinua uchumi wa wananchi wa eneo hilo.

Mkunda alisema kuwa moja ya mambo makubwa ambayo watayatekeleza ni pamoja na kurudishwa kufanya kazi kwa bandari ya Ujiji, kufanyiwa  ukarabati mkubwa wa soko la Ujiji ili kuwezesha wafanyabiashara kufanya biashara zao kwa tija lakini pia wamekubaliana na Mamlaka ya usimamizi wa usalama wa nchii kavu (LATRA) baadhi ya mabasi ya abiria kuanzia safari zake katika stendi ya Ujiji.

Katika mkutano huo Diwani huyo amekanusha uvumi ulioenea kwamba amekimbia kufanya siasa na kutekeleza majukumu yake kwenye kata hiyo na kukimbilia kuishi Dar es Salaam baada ya kukosa nafasi ya Umeya akieleza kuwa shughuli zake za biashara ndizo zilimfanya muda mwingi kuwa nje ya mkoa na kwamba yuko pamoja na wananchi wake kusimamia maendeleo ya kata hiyo kwa miaka yote mitano.

Mwisho.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3