Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
MCC MARY CHATANDA AOMBA KURA ZA EMANUELA MTATIFIKOLO ISIMANI

MCC MARY CHATANDA AOMBA KURA ZA EMANUELA MTATIFIKOLO ISIMANI

 


MJUMBE  wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MCC) Mary Chatanda, ameungana na mgombea wa CCM katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Ismani, Emmanuela Mtatifikolo, kwenye mikutano ya kampeni iliyofanyika katika Kata ya Itunundu kuelekea uchaguzi mdogo utakaofanyika tarehe 01 Juni 2026.

Chatanda ambae pia ni mwenyekiti wa umoja wa wanawake Tanzania (UWT) akizungumza na  wananchi waliojitokeza kwenye mikutano hiyo, Chatanda amesema amefika Ismani akiwa amebeba salamu za upendo kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Katika hotuba yake, Mary Chatanda amewahakikishia wananchi wa Ismani kuwa Emmanuela Mtatifikolo anazo sifa, uwezo na vigezo vinavyomwezesha kuwa mwakilishi mahiri wa wananchi wa Jimbo la Ismani.


Pia amewaomba  wananchi wa Kata ya Itunundu kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi ili kumpatia ushindi mgombea huyo wa CCM, akisisitiza kuwa CCM inaendelea kuamini katika viongozi wenye uwezo wa kuwatumikia wananchi na kuleta maendeleo endelevu katika jimbo hilo.

Kwa upande wake mgombea ubunge wa jimbo hilo Emanuela Mtatifikolo alisema kuwa anagombea ubunge jimbo hilo anatambua mahitaji yao na kuwa atatekeleza vema ilani ya CCM na kuendeleza yote yaliyoachwa na mtangulizi wake Marehemu Wiliam Lukuvi .

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3