Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
MBARONI KWA KUKUTWA NA MENO YA TEMBO

MBARONI KWA KUKUTWA NA MENO YA TEMBO

 

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

 Polisi mkoani Kigoma kwa kushirikiana na askari wa Mamlaka ya usimamizi Wanyamapori (TAWA) imemtia mbaroni mtu mmoja mkulima na  mkazi wa kijiji cha Rungwe Mpya wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma akiwa na vipande vitano vya mawe ya tembo.

 Kamanda wa polisi mkoa Kigoma,Filemon Makungu akitoa taarifa kwa waandishi wa habari mjini Kigoma alisema kuwa mtu huyo alikamatwa baada ya raia wema kutoa taarifa kuhusu uwepo wa mtu huyo kuwa na nyara za serikali bila kuwa na vibali.

 Kamanda Makungu alisema kuwa kwa sasa mtuhumiwa huyo ambaye jina lake limehifadhiwa anashikiliwa kituo kikuu cha polisi mjini Kigoma wakati upelelezi wa shauri hilo ukiendelea ili kuweza kumfikisha mahakamani 

Aidha katika tukio lingine Kamanda Makungu alisema kuwa polisi imemtia mbaroni mtu mmoja mkazi wa kijiji cha Mwakizega wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma kwa tuhuma za kutakatisha fedha bandia.

 Katika tukio hilo Kamanda huyo wa polisi mkoa Kigoma alisema kuwa mtuhumiwa alikutwa na noti za shilingi 10,000 zenye thamani ya shilingi 850,000 ambazo alikuwa anazitakatisha kwenda kwenye mawakala wa kutuma na kutoa pesa ili kuzituma kwa watu mbalimbali ndipo katika baadhi ya maeneo hayo wakagundua kuwa hizo ni fedha bandia na kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama na hivyo kukamatwa. 

Mwisho.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3