Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
ENZO MARESCA KUMRITHI GUARDIOLA MAN CITY

ENZO MARESCA KUMRITHI GUARDIOLA MAN CITY

 

Enzo Maresca aliondoka Chelsea mnamo Januari chini ya miezi sita baada ya kushinda Kombe la Dunia la Vilabu

Enzo Maresca anatarajiwa kuchukua nafasi ya Pep Guardiola kama meneja wa Manchester City kabla ya msimu ujao.

Kama tulivyoripoti Jumatatu mkufunzi mashuhuri wa City Guardiola anatarajiwa kuondoka katika klabu hiyo kufuatia mchezo wa Jumapili dhidi ya Aston Villa Uwanja wa Etihad, mechi yao ya mwisho msimu huu.

Kocha mkuu wa zamani wa Chelsea Maresca anapigiwa upatu kuchukua nafasi ya Mhispania huyo maarufu kwa msimu wa 2026-27.

Huku City wakijiandaa na kuondoka kwa Guardiola majira ya kiangazi kwa zaidi ya miezi sita, mazungumzo na Maresca yako katika hatua nzuri.

Kocha huyo aliye na umri wa miaka 46 anatarajiwa kutangazwa rasmi kuwa mrithi wa Guardiola muda utakapowadia.

Mtaliano huyo ambaye alishinda Kombe la Dunia la Vilabu na Ligi ya Conference na kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa wakati alipokuwa Stamford Bridge, ashawahi kufanya kazi na City.

Alikuwa msaidizi wa Guardiola wakati Man City iliposhinda mataji matatu 2022-23 na alishikilia jukumu muhimu katika chuo cha mafunzo ya soka ya ya klabu hiyo kabla ya kujiunga na kikosi cha kwanza.

Guardiola aliwahi kumsifia Maresca kama: "Mmoja wa makocha bora duniani. Ninamfahamu vyema Maresca, lakini kazi aliyoifanya Chelsea haijapewa uzito unaostahili.''


Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3