Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
DED MBEYA DC AISHUKURU SERIKALI AJIRA 259.

DED MBEYA DC AISHUKURU SERIKALI AJIRA 259.

 


Na Josea Sinkala, Mbeya.

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Erica Yegella, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutoa fursa ya ajira mpya takribani 259 katika kipindi cha mwezi Januari na Mei 2026 kwa Halmashauri hiyo.


Katika kipindi cha mwezi Januari, Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya ilipangiwa ajira mpya 111 kwenye kada tofauti ikiwemo elimu msingi na sekondari, afya, maendeleo ya jamii na utawala.


Hata hivyo Halmashauri hiyo imesema mnamo mwezi Aprili 2026, Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya ilipangiwa ajira mpya nyingine 118 kwenye kada tofauti ikiwemo elimu msingi na sekondari, afya, ujenzi na uhasibu.


Mwezi Mei, Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya ilipangiwa ajira mpya 30 mahususi kwa ajili ya watu wa kada ya afya pekee, wakataosaidia jitihada za utoaji huduma muhimu za afya katika zahanati na vituo vya afya vilijengwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.


Bi. Yegella amesema ajira mpya zilizotolewa kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kupitia Ofisi ya Rais Sekretarieti ya ajira katika Utumishi wa Umma ni jambo ambalo anapaswa kupongezwa sana Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kukubali ombi la kuongeza watumishi katika Halmashauri.


"Katika kipindi cha miezi mitano pekee, Rais ameruhusu Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kupangiwa ajira mpya zaidi ya 250. Tunamshukuru sana kwa hili. Hii ni fursa kwa vijana wa kitanzania pamoja Halmashauri kwani itasaidia kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma muhimu za kijamii," ameeleza Bi. Erica Yegella, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbeya.


Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3