DC SITTA APONGEZA UWEKEZAJI MKUBWA UJENZI WA HOTEL MPYA YA ISIMILA KATA YA MSEKE
NA MATUKIO DAIMA MEDIA
IRINGA.
MKUU wa Wilaya ya Iringa Benjamini Sitta asifu mradi ujenzi wa Hoteli ya Isimila iliyopo kata ya Mseke wilayani Iringa huku Hoteli hiyo ikitajwa baada ya kukamilika itaweza kutoa fursa kwa wasafiri kupata huduma nzuri ya chakula.
Akizungumza na Matukio Daima Media DC Sitta alisema kuwa kukamilika kwa Hoteli hiyo itasaidia kutoa ajira kwa vijana wa wilaya ya Iringa pia huduma ya chakula kwa safari .TAZAMA MAHOJIANO BOFYA LINK HII
DC Sitta alisema na kutazama ratiba kama itofaa mwenge kutembelea Hoteli hiyo lakini kutokana na ratiba kutokidhi wanatarajia kutakuwa na ujio wa viongozi mbalimbali ambao ambao watapata ratiba ya kwenda kuzindua na kuwatembelea ikiwa ni moja ya kuwatia moyo wawekezaji.
“Mradi wa Isimila hoteli ni mzuri na tulitarajia mwenye utakapofika Mkoani Iringa upite katika Hoteli hiyo kwa ajili ya kuzindua lakino ratiba imebana na tunatarajia viongozi wa kitaifa wanaoendelea kuja Iringa watapata nafasi hiyo”
“Hivi karibuni tumetoa fidia kwa wakazi wa Isimila stone Age kwa maana tunapata nguvu na kuvipa vivutio vya utalii nguvu hivyo tutaona namna ya kumsapoti mwekezaji”alisema
Aidha katika ujio wa mwenge au kiongozi yeyote wa kitaifa kutaweza kumpa uwanja wa kuonekana na kutambulika,Kwa sababu uwepo wa wawekezaji unaleta manufaa katika jamii na vile vile katika mchango mkubwa wa pato la Taifa.
Hotel ya Isimila inatarajia kuhudumia mabasi zaidi ya 20 na abiria 1126 kwa wakati mmoja hii itakuwa ni Hotel kubwa katika barabara kuu ya Iringa -Mbeya na Mbeya -Dar es Salaam kuhudumia idadi kubwa ya abiria kwa wakati mmoja .

