Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
CHANJO YA EBOLA HUENDA IKACHUKUA MIEZI TISA, WHO YAONYA

CHANJO YA EBOLA HUENDA IKACHUKUA MIEZI TISA, WHO YAONYA

 

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema huenda ikachukua hadi miezi tisa kabla ya chanjo dhidi ya aina ya Ebola inayosambaa kwa sasa kuwa tayari.

Chanjo mbili ambazo zinazoweza kutumika dhidi ya Ebola ya Bundibugyo zinatengenezwa, lakini hakuna hata moja ambayo imefanyiwa majaribio ya kitabibu kufikia sasa,hii ni kulingana na mshauri wa shirika la WHO, Dkt Vasee Moorthy.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dkt. Tedros Adhanom, amesema kumekuwa na visa 600 vya Ebola na vifo 139 kutokana na ugonjwa huo, huku idadi hiyo ikitarajiwa kuongezeka.

WHO ilitangaza hali ya dharura ya afya ya umma ya kimataifa, lakini ikasema hali hiyo bado haijafikia kiwango cha kuwa janga la dunia.

MWISHO.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3