Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
CCM IRINGA WAZINDUA KAMPENI UCHAGUZI MDOGO ISIMANI WAKIMSIFU MGOMBEA WAO MTATIFIKILO

CCM IRINGA WAZINDUA KAMPENI UCHAGUZI MDOGO ISIMANI WAKIMSIFU MGOMBEA WAO MTATIFIKILO


NA MATUKIO DAIMA MEDIA.

CHAMA cha Mapinduzi (CCM)MKoa wa Iringa  kimezindua kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Isimani na kumwaga sifa kwa mgombea wa chama hicho Emmanuela Mtatifikolo,wakieleza kuwa anastahili kutokana na uwezo wa kazi zake za kusimamia miradi ya maendeleo nchini.


Uzinduzi wa kampeni hizo ulifanyika jana katika kata ya Itunundu, Tarafa ya Pawaga ukihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama, wafuasi wa chama hicho pamoja na wananchi wa maeneo mbalimbali pamoja na wabunge wa mkoa wa Iringa wakionyesha mshikamano katika uchaguzi huo.


Akizungumza katika uzinduzi huo,  mjumbe wa kamati kuu ya CCM Taifa, Salim  Asas amewataka wanachi wa jimbo la Isimani kumuamini Mgombea Ubunge wa jimbo hilo Emmanuela Mtatifikolo kwa sababu sifa anazo na uwezo kwa kulijenga jimbo la isimani anao.


Asas alisema kuwa hawajaenda Isimani kwa ajili ya kumnadi mgombea ili aingie bungeni kwa maneno ya kisiasa bali mgombea anasifa kutokana na kazi zake na weredi wa kutatua changamoto za wananchi. 


Alisema kuwa ana mfahamu Emmanuela tangu uchaguzi wa 2020 ambapo kamati kuu ya halmashauri ya taifa ilimteua kuwa mratibu wa uchaguzi kanda ya nyanda za juu kusini.


Alisema kuwa Emmanuela aliweza kuratibu majimbo yote yaliyopo nyanda za juu kusini ambapo ina majimbo zaidi ya 40 na kata 450.


“Kazi aliyoifanya huyu dada mpaka leo sijawahi iona kuratibu majimbo 40 na kata 450, je atashindwa jimbo la Isimani?na wakati huo kila anapoenda anawauliza wagombea je jimbo hilo lina shida gani ili akija mgombea uraisi aweze kumueleza na ikifika jioni anandika, alienda kijiji kwa kijiji, kata kwa kata, jimbo kwa jimbo”alisema


Alisema kuwa kwa jimbo la isimani kama kuna eneo watasema kuna tatizo la barabara Emmanuela anajua nini maana ya shida  ya barabarakwa sababu hakuwa mtu wa mjini mjini, ni mtu wa vijijini



“Mimi ni mdau wa maendeleo wa jimbo la Isimani nilitoaa ahadi kwamba katika mkoa wa iringa tutawezeshana katika kila kata kuwe na ofisi ya chama,je kuna kata jimbo la isimani haina ofisi ya chama? Alihoji,Na kusema kuwa endaapo watamkabidhi jimbo Emmanuela bado wataendelea kushirikiana”alisema Salim


Aliongeza kuwa kwa uzoefu alioonyesha na uzoefu alionao wana Isimani hawapaswi kuwa na wasiwasi wowote sio kwa maana ya kumnadi ili awe mbunge wala kupamba bali anasifa zinazo jionyesha  kutokana na matokeo ya kazi yake.


Kwa upande wake, Mwenyekiti ya CCM Mkoa wa Iringa Daud Yasin alisema kuwa mgombea hyo ni mnyenyekevu, msikivu na mwenye nidhamu,hivyo akichaguliwa ataweza kusaidia kusukuma mbele maendeleo ya wananchi wa isimani.


“Emmanuela ni mnyenyekevu, mtii na anasikiliza tukawahimize wananchi wakajitokeze kwa wingi kupiga kura”alisema Yasin


Akizindua kampeni hizo, Mjumbe wa kamati kuu ya CCM Taifa na mlezi wa CCM Mkoa wa Iringa Mohamed Aboud wakati wa uzinduzi wa kampeni Chama cha Mapinduzi Jimbo la Isimani na kuwataka wana Isimani kujitokeza kwa wingi kwenda kupiga kura June 1,2026 wasiishie kusema chama kimeshinda au Emmanuela kashinda wakati hawajapiga kura.


Alisema kuwa kamati ilikaa na kujua kuwa Emmanuela atavaa viatu vya Lukuvi na kwamba mgombea huyo amejipanga kushughulikia changamoto zote za wana isimani.


"Niwahakikishie baada ya kumchagua Emmanuela ndani ya miezi sita mtaona matokeo ya juhudi zake na utendaji kazi wake na mtaamini kuwa viatu vya Lukuvi vimemtosha sawa sawa" alisema


Alisema kuwa moja ya mambo amabayo anatakiwa kuyaendeleza ni pamoja na ujenzi wa barabara ya Pawaga hadi Iringa mjini,skimu ya umwagiliaji pamoja na kilimo na ufugaji sambamba na yale yote ambayo Marehemu Lukuvi aliyaanza na kuyaacha bila kukamilika.


Katika hatua nyingine,viongozi waliokuwa wamejitokeza kuwania ubunge kupitia kura za maoni za CCM walionyesha mshikamano kwa kuungana na kumuunga mkono mgombea huyo.


Aliyekuwa mtia nia wa ubunge jimbo hilo,Festo kiswaga alisema mara baada ya jina la Emmanuela kupitishwa na chama, walimpongeza na kusisitiza kuvinja makundi ndani ya CCM.

Kwa Upande wake Mgombea Ubunge wa Jimbo hilo Emmanuela Mtatifikolo alisema kuwa amepokea mikoba ya Lukuvi akiamini kuwa anaweza kutenda zaidi ya alivyofanya marehemu Lukuvi.


Alisema kuwa aliamua kwenda kugombea katika jimbo hilo baada ya Kifo cha Lukuvi watu wengi walipata wasiwasi na kujiuliza itakuwaje ndipo akaamua kurudi nyumbani kugombea ili kuwatoa wasiwasi wana Isimani.


" Wakati wa kifo cha Marehemu Mh Lukuvi wananchi wengi walikuwa na majonzi na huzuni ya kuondokewa na mpendwa wao wakati huo wanajiuliza itakuwaje nani atabeba mikoba,ndipo nikaamua kuja kugombea kwa sababu nina uwezo wa kukabiliana na changamoto za jimbo hili"


“mimi sina maneno mengi napenda matokeo zaidi hivyo naomba mnichague kwa kura nyingi ili niwatoe wasiwasi wa maendeleo katika jimbo hili”alisema


Mtatifikolo aliongeza kuwa anaishukuru serikali ya CCM chini ya uongozi wa Lukuvi kwa kuliongoza jimbo la Isimani kwa miaka 30 imefanya kazi kwa bidii na kuleta maendeleo katika jimbo hilo.


Akizungumzia maendeleo yaliyopatikana katika upande wa afya alisema kuwa awali wananchi walikuwa wanafariki kwa kukosa maji mwilini jambo ambalo Lukuvi alitatua kwa kupeleka huduma za afya,zahanati na vituo vya afya ambavyo vinaendelea kujengwa.


“Serikaliya awamu ya sita imeleta miradi mingi ya maendeleo ikiwemo afya, maji, uchumi pamoja na miundo mbinu ya barabara”


Akizungumzia suala la uchumi Mtatifikolo alisema kuwa atahakikisha wana pawaga wananufaika na zao la mpunga kwa kulisha nchi pamoja na nchi za jirani kwa kuwatafutia soko la uhakika.


Katika upande wa barabara alisema atahakikisha barabara ya Isimani Izazi, inajengwa kwa kiwango cha lami sambamba na barabara ya pawaga Iringa mjini ambao tayari Mbunge wa Iringa mjini Fadhili Ngajilo na Lukuvi waliisha iombea fedjha za ujenzi ikiwa pamoja na kukamilika kwa wakati.


“Nimekabidhiwa mikoba ya Lukuvi hivyo nimejipima na kuona natosha sana kuweza kutimiza yale yote ambayo alitamani wana Isimani wayapate,sambamba na kutekelza ilani ya chama, lakini haya yote hayawezi kufanikiwa kama hamtapiga kura june 1,2026”alisema


Uchaguzi huo mdogo wa ubunge jimbo la Isimani unafanyiks kufuatia aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo William Lukuvi kufariki dunia,hali iliyowalazimu tume ya taifa ya uchaguzi kutangaza nafasi hiyo kuwa wazi na kuitisha uchaguzi mdogo.


Mbali na CCM, jumla ya vyama 17 vya upinzani vimejitokeza kushiriki uchaguzi huo.

MWISHO.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3