WENGI WAJIUNGA NA VUNJA BEI BETE
NA MATUKIO DAIMA MEDIA
Kampuni ya Vunjabei Group chini ya Mtendaji Mkuu wake, Fred Ngajiro maarufu kama Fred Vunjabei, leo imezindua rasmi jukwaa jipya la michezo ya kubahatisha lijulikanalo kama Vunjabei Bet, ambalo limeanza shughuli zake hapa nchini Tanzania huku likiwa na mpango wa kupanua huduma zake katika nchi saba za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Fred Vunjabei amesema mafanikio ya awali ya jukwaa hilo yamekuwa makubwa kuliko walivyotarajia, ambapo ndani ya wiki moja pekee tangu kuanza kwa usajili, zaidi ya watu laki moja na elfu themanini wamejiunga na huduma hiyo.

"Ilionekana ni mwanzo mgumu kufikiria Vunjabei Bet itaanzaje, lakini mpaka sasa tumepokea usajili mkubwa sana ndani ya wiki moja tu. Tunawashukuru Watanzania kwa kuipokea vizuri huduma yetu," amesema Fred Vunjabei.
Ameongeza kuwa lengo lao ni kufikisha zaidi ya watumiaji milioni tano katika siku zijazo, huku akisisitiza kuwa ukuaji wa kampuni hiyo haujatokana na bahati bali umetokana na maono, nidhamu, ubunifu pamoja na kujituma kwa timu yao.