WAFANYABIASHARA WATAHADHARISHWA UDANYANYIFU WA VIPIMO BIASHARA ZA KUVUKA MPAKA
Na Fadhili Abdallah,Kigoma
WAFANYABIASHARA na wawekezaji wanaozalisha bidhaa mbalimbali kwa ajili ya soko la nchii za ukanda wa maziwa makuu wametakiwa kuacha udanganyifu na kuzingatia vipimo sahihi vya bidhaa zao ili kuzifanya bidhaa hizo kuaminika kwenye soko la Kimataifa.
Meneja wa Wakala wa vipimo mkoa Kigoma, Laurent Kabikiye alitoa tahadhari hiyo wakati wa kungamano la biashara na uwekezaji la ziwa Tanganyika lilomalizika mwishoni mwa wiki mjini Kigoma na kubainisha kuwa kuzingatia vipimo sahihi vya ujazo wa bidhaa kunachochea maendeleo.
Kabikiye alisema kuwa fursa iliyojitokeza kwenye kongamano hilo inaweza isiwe na maana kubwa hapo baadaye na biashara ikashindwa kufanyika kwa mafanikio kama wafanyabiashara na wawekezaji watashindwa kuzingatia viwango vya ubora wa bidhaa na vipimo halisi vya ujazo wa bidhaa hizo,
Baadhi ya wawekezaji waliohudhuria kongamano hilo ikiwemo kampuni ya Crown Royal Van Baverages Tanzania inayotengeneza vinywaji vya tangawizi na pombe kali kwa ajili ya soko la maziwa makuu imebainisha kuwa ni muhimu kuzingatia kwa viwango vilivyoweka na shirika la viwango nchini (TBS) na vipimo halisi vya bidhaa vinavyotambuliwa na wakala wa vipimo nchini.
Operesheni Meneja wa kampuni hiyo alisema kuwa bidhaa zinazozingatia ubora kwa nchi ambayo bidhaa inapelekwa sambamba na kuzingatia ujazo halisi ulioandikwa kwenye bidhaa husika inaipa thamani bidhaa hiyo na kukubalika na kuaminika kwenye soko.
Naye Mjasiliamali Angelina Patrick kutoka kampuni ya Angelina Food Proccesing ya Mjini Kigoma alisema kuwa kongamano limefanikiwa na kufungua fursa kwao ya biashara na wenzao wa nchi za ukanda wa maziwa makuu ambapo pamoja na hilo alisema kwamba elimu ya kuzingatia ubora wa bidhaa na ujazo halisi wa bidhaa imekuwa moja ya faida kubwa ya kongamano hilo.



