UMUHIMU YA SIKUKUU YA WAFANYAKAZI DUNIANI.
NA Ester Sebastian (UOI) Matukio Daima.
Baadhi ya wafanyakazi wa mkoa wa Iringa wameelezea umuhimu wa mei mosi ambayo kila mwaka inafanyika mara moja ya tarehe moja mwezi wa tano.
Mmoja wa mfanyakazi, Irene Lucky akieleza Matukio Daima umuhimu wa sikukuu ya wafanyakazi Kuwatambua na kuwaheshimu wafanyakazi kwa mchango wao katika maendeleo ya jamii na uchumi.
"Umuhimu wa sikukuu ya Wafanyakazi kuwatambua wafanyakazi duniani na huwapa heshima wafanyakazi kwa kazi zao za kila siku zinazochangia maendeleo ya uchumi na jamii." Alisema Lucky.
Naye Peter Kitita amesema umuhimu wa sikukuu ya wafanyakazi duniani Kupigania haki za wafanyakazi, kama mishahara bora, mazingira salama ya kazi, na saa za kazi zinazofaa Kukuza haki za wafanyakazi.
"Siku ya wafanyakazi duniani inawapa nguvu kutambua haki zao kama mishahara mzuri, mazingira salama ya kufanyia kazi maana kuna baadhi ya wafanyakazi hivyo vitu vimekosekana katika sehemu zao za kazi" Alisema Kitita.
Kwa upande wake, Elizabeth Fannuely amesema Kwa kuwa ni sikukuu ya kitaifa katika nchi nyingi kama Tanzania, wafanyakazi hupata muda wa kupumzika na kurejesha nguvu ama Kukuza mazungumzo kati ya wafanyakazi na waajiri ni nafasi ya kujadili changamoto za kazi na kutafuta suhuhisho bora.
"Sikukuu ya kitaifa katika nchi kama Tanzania wafanyakazi kuwapa mda wa kupumzika na kukuza mazungumzo kati ya wafanyakazi na waajiri na kutatua changamoto mbali mbali kwa kupata hitimisho bora katika utendaji wao wa kazi zao" Alisema Fannuely.
Serikali hutambua umuhimu mkubwa ya Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani kwa sababu siku hiyo ina mchango wa moja kwa moja katika ustawi wa nchi na wananchi na kuimarisha ustawi wa wafanyakazi na maendeleo ya taifa kwa ujumla

