Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
SIRRO AKEMEA KUCHELEWA  MRADI WA UMEME IGAMBA

SIRRO AKEMEA KUCHELEWA MRADI WA UMEME IGAMBA

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

Mkuu wa  mkoa wa Kigoma Balozi Simon sirro ameeleza  kutoridhishwa na kasi ya utekelezaji  wa mradi wa  kufua umeme katika Mto Malagarasi eneo la Igamba wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma akiitaka kampuni inayotekeleza mradi huo kufanya kazi kulingana na mkataba wao vinginevyo serikali itachukua hatua.

Balozi Sirro alisema hayo alipotembelea mradi huo na kusema kuwa ametembelea mradi huo mara kadhaa lakini kasi ya utekelezaji wa mradi huo imekuwa ndogo wakati mradi unapaswa kukamilika mwakani na kazi iliyofanyika haijafika hata nusu.

Alisema kuwa utekelezaji huo duni wa mradi unatokana na kutokuwepo kwa eneo la ujenzi kwa vifaa muhimu ambavyo vingefanya mradi huo kwenda kwa kasi na kwamba ofisi yake inatathmini na kuona hatua za kuchukua katika kukabiliana na changamoto hiyo.



Pamoja na kushindwa kutekeleza mradi huo kwa wakati Mkuu huyo wa mkoa ameishutumu kampuni ya Ddongfung Electric International Corporation kuleta ndugu na jamaa zao katika kazi zinazoweza kufanywa na Watanzania ikikiuka pia taratibu za kisheria za kuajiri watumishi katika mradi huo.

Akizungumza wakati za ziara hiyo Mkuu wa wilaya Uvinza,Dinah Mathamani alisema kuwa mradi bado upo nyuma ukiwa ni asilimia 24 ya utekelezaji ukiwa nyuma hivyo hatua Zaidi za kumbana mkandarasi zinahitajika ili aweze kuongeza spidi.

Awali Msimamizi wa mradi huo, Mhandisi Philip Malila kutoka TANESCO alisema kuwa mradi huo ni Mega Watt 45 zinazotarajia kuzalishwa katika eneo hilo ukitarajia kukamilika Oktoba 2027 na kwamba kiwango hicho cha Umeme kitachangia katika grdi ya Taifa.

Mwisho.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3